06.01.2019 | HAPPY KWAYA NI WATUMISHI WA MUNGU WANAOGUSA MAISHA YETU KWA HUDUMA YAO YA UIMBAJI TUZIDI KUWAOMBEA.

Kila tunaposikia nyimbo za hawa watumishi wa Mungu wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" (Happy Kwaya) tunabarikiwa sana, tunainuliwa imani zetu, tunaburudika, tunajifunza kupitia ujumbe wao, tunapata nguvu mpya za kusonga mbele katika kazi ya Mungu na tunapata ujasiri wa namna ya tofauti sana. Nyimbo zao zimejaa mafuta ya upako, unaposikia unahisi mbingu inashuka, uwepo wa Mungu unakuzunguka. Hakika Mungu anawatumia watu wake hawa kwa njia ya tofauti sana. Siku ya Jumapili 05.01.2019 wametubariki sana katika ibada ya Kupeleka Mahitaji Yetu kwa Mungu iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Tuzidi kuwaombea katika huduma yao ya uimbaji, kazi zao, familia zao, mahusiano yao, masomo yao, afya zao na kila wanachofanya kikafanikiwe kwa ukubwa. Mwaka 2019 ukawe ni mwaka wao wa mafanikio katika uchumi wao na huduma yako ya uimbaji. Mungu akainue vipaji vingine ndani yao. 


Kama unaguswa na huduma yao naomba sasa utamke maneno machache kwaajili ya maisha yao na Mungu atakubariki kwa maombi yako utakayofanya dakika hii. Asante.

-------------

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.
Mlima wa Moto Mikocheni "B"



































Comments