06.01.2019 | MATUKIO KATIKA PICHA KATIKA KIPINDI CHA KUSIFU NA KUABUDU SIKU YA JUMAPILI.

Haya ni matukio katika picha ya Maombi na maombezi yalivyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 06.01.2019 kwenye ibada ya KUPELEKA MAHITAJI YETU. Maombezi haya yalifanyika mara baada ya ibada ya kusifu na kuabudu iliyoongozwa na mzee wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" Martha Komanya kumalizika kuongoza kipindi hicho cha kusifu na kuabdu. 
Martha Komanya


Wachungaji wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na Mch. John Mhina kutoka Kenya walingia vitani kupambana na roho chafu zilizoharibu maisha ya watu kwa mwaka 2018 na kusababisha maisha ya watu kuwa ya ovyo ovyo. Ilikuwa ni ibada iliyojaa nguvu za Mungu na watu wengi sana waliguswa na nguvu za Mungu pale walipojiachia kwa Mungu aliye hai na kupeleka maombi yao kwao huku wakilia machozi. Hakika Mungu wetu wa mbinguni alionekana akituhudumia kwa njia ya tofauti sana, wingu lake lilitufunika, malaika wake walituzunguka pande zote na tuliona uwepo wa Mungu na nguvu za Mungu. 



Tunakushukuru sana kwa kushiriki ibada hii ya kihistoria kwako. Wiki hii Mungu ataonekane katika maisha yako na kila sehemu utakayokuwepo ukihangaika na maisha. Mungu akabariki kazi ya mikono yako na akuondoleee udhaifu katika mwili wako.

Jiamini na BWANA atafanya wepesi katika kazi zako, BWANA atashughulika na afya yako pamoja na changamoto ulizovuka nazo mwaka 2018 kuelekea mwaka 2019. Kumbuka huu ni mwaka wa ONGEZEKO NA MAFANIKIO katika uchumi wako, huduma yako, afya yako, masomo yako, kazi zako n.k, kwahiyo kaa ukitegemea BWANA kufanya jambo katika maisha yako. 
Unachotakiwa ni kuwa vizuri na Mungu wako, kufanya kazi kwa bidii, kuomba na kufunga, kumtafuta Mungu kwa viwango vya tofauti sana, kutenda mema na kuacha kujichanganya na ya dunia, kuwa mtu wa vitendo sana kuliko maneno mengi yasiyo na faida kwako, kuacha na mabaya na yasiyompendeza Mungu. Nakupenda na ninakutakia siku njema na siku ya Jumatatu kutakuwa na ibada ya Kuvunja laana na mameno mabaya uliyotamkiwa kutoka kijijini kwako, kwahiyo njoo na karatasi au kitambaa kilichoandikwa jina la kijijini kwako nasi tutakuombea na utafunguliwa na kuwa mbali na laana 2019, ibada itaanza saa 9 alasiri.






































































Comments