06.01.2019 | JOYBRINGERS KWAYA YASHNGAZA KATIKA IBADA YA JUMAPILI

Joybringers Kwaya kwa kweli mmetubariki sana katika ibada ya Kupeleka Mahitaji Yetu Kwa Mungu iliyofanyika siku ya Jumapili 06.01.2019 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Victor Aron hakika umeonyesha kiwango chako katika uimbaji pale ulipoimba "Live" na waimbaji wenzako. Sauti zenu na jinsi mnavyomsifu Mungu vinatubariki sana. Kupitia nyimbo zenu watu wanamjua Mungu, wanamrudia Mungu, wanaiunua viwango vyao vya imani, wanajitakasa, wanapata nguvu mpya ya kusonga mbele, wanaachana na dhambi. Mungu azidi kuwatumia kwa viwango vingine mwaka 2019, nasi tunategemea kuinuliwa kupitia huduma yenu hii ya uimbaji kwa maana Mungu wetu hukaa katikati ya sifa. Nina wapenda sana watoto wa Mungu wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Wewe ambaye hukabahatika kushiriki ibada ya Jumapili hii tunakualika katika ibada ya kuvunja laana na mabaya uliyonenewa na watu wasiokupenda kutoka kijijini kwako ili usifanikiwe hapa mjini au mahali unapoiishi. Wapo watu hawatamani kukuona unaishi mjini na ukifanikiwa bali wanatamani urudi kijijini na ukaishi maisha ya dhiki kama wao na mbaya zaidi usimtumikie Mungu. Jumatatu hii njoo na kitambaa chako au karatasi lako likiwa limeandikwa jina la kijiji unachotoka. Ibada itaanza saa 9 alasiri kutakuwa na mhubiri kutoka Kenya Mch. John Mhina nikishirikiana na wachunagaji wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Mlima wa Moto Mikocheni "B"






















Comments