23.12.2018: NINI MAANA YA KRISMASI?

NINI MAANA YA KRISMASI?
Kabla ya ujumbe wa Mungu wa siku ya leo, natamani nikusalimie “Mery Christmas, heri na Baraka za Krismasi 2018.” Tunamshukuru Mungu tumeona Krismasi ya mwaka 2018. Ukipata muda soma Mathayo 1:18-19, Luka 2: 1- 40 na Isaya 9:6-9 utapata kujua maana ya Krismasi. Tafakari maswali yafuatayo katika siku ya kipindi hiki cha kuzaliwa BWANA wetu Yesu Kristo. Je, Unajua maana ya Krismasi? Je, unapata nini kwenye Krismasi? Mungu anataka nini siku hii ya Krismasi? Je, Una jambo gani lakumwambia Mungu siku ya Krismasi? na Utanipa nini Mungu siku hii ya Krismasi?

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

UNAPOSHEREKEA KRISMASI UWE NA MAONO YA KIROHO

Tunaposherekea Krismasi ninaomba uwe na maono ya Kiroho, kwasababu Krismasi sio kula pilau, kuvaa nguo mpya tu. Krismasi ina maana zaidi Kiroho. Tunakula na kuvaa siku ya Krismasi kwasababu ni sikukuu lakini lengo lake kuu sio kula na kuvaa. Kipindi hiki cha Krismasi Pamba undani wako, pamba kiroho chako, anza upya kuishi maisha ya Kiroho.”
 Krismasi ni sikukuu ambayo inapambwa zaidi kuliko sikukuu zote duniani, ni sikukuu ambayo haina dini, watu wote wanasherekea Krismasi. Watu wanapamba mahoteni, mahospitalini, kwenye mabenki na kwenye majumba yao kwaajili ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Utakuta siku ya Krismasi kuna mapambo mengi sana na watu wanagombania miti ya Krismasi ili waweze kupamaba kwasababu aliyezaliwa amefanya ulimwengu uzizime, maana ni uthibitisho wa upendo wa Mungu kwa wanadamu. 

Ukisoma Yohana 3:16 inasema, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu mpaka akamtoa mwanae wa pekee ili kila amwaminie apate uzima wa milele.” Hakuna sikukuu inayosherekewa na watu wengi kwa kiushabikia kama Krismasi, utakuta watu wanahangaika kutafuta chakula, nguo za kuvaa kwaajili ya Krismasi. 



KRISMASI NI SIKU AMBAYO ILIBADILISHA KALENDA.

Tutanatambua ya kuwa Krismasi ni siku ambayo ilibadilisha kalenda ya ulimwengu mzima. Kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo walikuwa wakisema “AD maana yake Before Christ (Kabla Ya Yesu). Alipozaliwa Yesu wakaanza kuhesabu mwaka wa kwanza, wa pili na sasa ni miaka 2018. Hakuna mtu aliyeweza kubadilisha kalenda. 
Haijalishi mwaka ni mfupi au mrefu bado watu wanaanza kuhesabu tarehe 1 Januari hadi 30, 2 Februali hadi 29 au 28, wanaendelea mpaka kufika 1 Desemba hadi 30 lakini baada ya kuzaliwa Kristo wakabadilisha wakasema, “Baada ya Kristo”.



BABU SIMON ALITAMANI KUFA BAADA YA KUMUONA YESU.

Unatakiwa kutambua kuwa sikukuu ya Krismasi ilitangazwa na malaika, na haikutangazwa na mtangazaji wa TBC, ITV, wala sio magazeti lakini ilitangazwa na malaika kutoka mbinguni na kusema “Amezaliwa Yesu Kristo.”
 Hii ni sikukuu ya ajabu sana duniani kote. Ukisoma Luka 20 utaona Simon alikuwa akingojea kuzaliwa kwa Yesu Kristo, na alipozaliwa na kukua, alimshika mkono, na baada ya kushikwa Simon akasema, “Sasa ninatastahili kufa kwa maana macho yangu yameona Utukufu wa BWANA, wokovu wa BWANA na mtoto huyo atakuwa ni anguko au inuko kwa wengi.”

Katika maisha yangu sijaona mjukuu anazaliwa halafu babu anakufa siku hiyo hiyo. Ninachojua ni kwamba wajukuu ni furaha kwa wazee. Lakini mjukuu Yesu Kristo alileta maajabu mpaka akasababisha babu Simon kusema, sasa nife nipumzike kwa maana nilichokuwa nangoja nimekiona, nilikuwa natamani kumuona Yesu na leo nimemshika mkono. 
Na hii ilitokea baada ya babu Simon kwa muda mrefu kumsubiri Yesu amuone kwa macho yake, na alipomuoa akasema hata akifa haina shida maana ameshamuona Yesu.



JE, UNGEPENDA MUNGU AKUTENDEE NINI KIPINDI CHA KRISMASI?

Mwaka huu wa 2018 ungependa Mungu akufanyie nini kipindi hiki cha Krismasi? Ungependa Mungu akupe nini Krismasi hii? Inasikitisha kuona watu wengi wanatamani kupata vitu vidogo baada ya Krismasi na wanajisahau kutamani kupata vikubwa kutoka kwa Mungu. Watu wengine siku ya Krismasi wanaishia kulewa sana na kulala kwenye mitalo. 
Watu wengi wanalewa na wanaishia kupata ngeu baada ya kupigana, wengine wanaishia maugomvi katika ndoa eti kwasababu wanae hawajapata nguo mpya za kuvaa siku ya Krismasi. Ninaomba kipindi cha Krismasi watu msigombane kwenye majumba. Krismasi ni kumkaribisha Yesu Kristo kwa upya, Krismasi ni birthday ya Kiroho.



TAFAKARI KWA MWAKA MZIMA UMEFANYA NINI MBELE ZA BWANA?

Tafakari kwa mwaka mzima mahudhirio yako ya ibada yalikuwaje? Utoaji wako wa sadaka kanisani ulikuwaje? Tengeneza maisha yako kwani ipo siku utakufa na utaulizwa ulifanya nini huko duniani, maisha yako yalikuwaje?. Mungu anatuona na anatuangalia, Mungu anatushangaa. 
Mungu anasema, “Mbona watu wangu hawaombi!” Mimi kama Bishop Dr. Gertrude Rwakatare huwa nashangaa napoona watu wako kimia hawataki kuja kufanya maombi ili BWANA awasaidie, watu hawapendi kufanya kazi ya Mungu wako “busy” na maisha. Kwa mwaka huu naomba uanze kuwaleta watu kwa Yesu na kutenda yaliyo mema kwa maana siku ya mwisho BWANA atakuuza; “Ulifanya nini duniani kwaajili yangu?



KIPINDI CHA KRISMASI TAMANI VIKUBWA NA SIO VIDOGO

Soma hadith hii, Kuna bilionea fulani alimchukua mtoto wake kipenzi siku ya Krismasi akampeleka kwenye “mall” yaani “supermarket” kubwa za Ulaya. Yule Bilionea akamwambia mwanane “Nenda ukanunue unachotaka.” Unataka nini mwanangu mimi baba yako ni Bilionea. Yule mwanane Ruth akaingia kwenye “Supermarket” na alipoona viatu akamjibu baba yake akasema, “No dady I have enough shoes”, nina viatu vya kutosha sihitaji viatu tena; Baba yake akampeleka kwenye eneo la maguni mazuri na alipofika pale Yule mtoto akasema, “I have enough dresses dady”, nina magauni yakutosha. Yule Bilionea akashangaa kuona mwanae hataki magauni, akampeleka kwenye madoli makubwa mazuri, yuke mtoto akaenda kuchukua kimdoli kidogo kinaimba, “Mammy...Mammy...Mammy..!!” akakichukia kile kimdoli kidogo na kumwambia baba yake bilionea, “Daddy I want this dolly .” 
Baba yake akashangaa kuona amechukia kimdoli kidogo sana na thamani yake ni dola 10. Yuke Bilionea akasema, “Yaani mimi baba yako nimekuja na mihela mingi inaniwasha na wewe unataka kamdoli. Mwanae akamwabia baba yake tajiri, “Buy”, Yule baba yake akamnunulia. Basi Yule mtoto akarudi nyumbani na kale kamdoli kanalilia “Mammy…mammy…mammy…” , si unajua watoto wanavyopenda midoli. Yule mtoto akawa anafurahia kile kimdoli kinavyosema “Mammy” kwasababu na yeye hufurahia anapomuitaga mama yake mzazi “Mammy”Kupitia mfano huu, ndivyo lilivyo kanisa la leo, wakati wa Krismasi hamtaki makubwa mnataka madogo, Mungu na walimwengu wanatushangaa, kwanini watu wanalilia pilau na nguo tu siku ya Krismasi? Pilau unaweza kula siku yoyote lakini siku ya Krismasi ni siku ya tofauti kwako, omba kitu kikubwa cha Kiroho. 
Mungu anashangaa unapolillia gauni siku ya Krismasi; gauni unaweza kununua siku nyingine, lakini siku ya Krismasi ni “special” tafuta kitu kingine kikubwa cha kiroho. Mungu anashangaa watu wanapolilia bia, wanapigana na kupasuana na chupa, damu zinawavuja, Mungu anasema, “Ninawashangaa hawa. Kwasababu Krismasi ”is not fighting”, sio kulewa, bali Krismasi ni siku ya mambo ya rohoni ya kutakasa moyo wako, kutengeneza “speed” yako” na Mungu. Mbona naona umepoa, huendi sawa na Mungu, mbona njaa na kiu ya kumtafuta Mungu haipo, mbona husomi Neno la Mungu tena? Mungu anataka ubadilishe maisha yako.



KIPINDI CHA KRISMASI NI KIPINDI CHA KUSAMEHEANA

Mungu anategemea Krismasi hii watu tusameane, Dr. Stahimili amesema katika maelezo yake kuwa, “Kama kuna mtu amekukwaza, amekukosea basi msamehe.” Krismasi maana yake ni kusamehe na kusahau, sio kukumbuka ya zamani. Unatakiwa kujua kuwa aliyekuudhi ni mwanadamu ila Yesu hajakuudhi, usiahame kanisa eti kuna mtu anakuudhi. Unatakiwa kujua kuwa aliyekuudhi hana mbingu wala mahali pa kukupeleka. Kanisani ni mahali pa Yesu, kila mtu ana haki yake katika kanisa. Kwahiyo tengeneza maisha yako kwa kusamehe na kusahau yale uliyotendewa vibaya.



Wakati wa Krismasi ni wakati wa upendo, wenzetu wazungu siku ya Krismasi wanaonyeshea kadi, wanatoa zawadi na kuweka chini ya mtu wa Krismasi, utakuta maboksi ya zawadi yamejaa zawadi na siku ya tarehe 26 Desemba ni siku ya kufungua zawadi, wanaita “Boxing day”.

Kwahiyo Krismasi ni wakati wa kumuwazia mtu ana nini nyumbani kwake, onyesha upendo kwa ndugu yako aliyooko Kigamboni au aliye mbali na wewe, mpigie simu na umsalimu, mtumie kitenge. Wakati wa Krismasi ni kutafuta amani na watu wote.. Waebrania 12:14



BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE ALIVYOFANYA MAOMBI KUINGIA MWAKA 2019 NA KUSHEREKEA KRISMASI.

Baba katika jina la Yesu Kristo tunaposhererkea Krismasi ninaomba katika Jina la Yesu Kristo ukaingia tena mioyoni mwetu, tunajikabidhi tena upya kwako Mungu Mtakatifu utupe tena mwaka 2019, mwaka wa kazi, mwaka wa kiroho, uliojaa Baraka ili tukutumikie Mungu wetu uliye juu ili nasi tuwe Baraka kwako. Katika jina la Yesu ninamkabidhi mmojammoja kwako



MHUBIRI: Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

TAREHE: Jumapili 23.12.2018

MAHALI: Mlima wa Moto MIkocheni “B”

UJUMBE: Kupokea Habari Njema




































































Comments