28.10.2018: NINAAMINI MUNGU ATANIPONYA KIDONDA SUGU BAADA YA MAOMBI.

Kwa mara ya kwanza huyu kaka aliweza kukanyaga katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 28.10.2018 katika ibada ya maombi ya hatari akihitaji kufanyiwa maombi ili aweze kupona kidonda sugu kilichomtesa kwa muda wa miaka mitano (5), alikuwa na haya ya kusema, 


"BWANA Yesu asifiwe. Ninamshukuru Mungu kwa rafiki yangu aliyeweza kunisaidia kufika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” kwa mara yangu ya kwanza baada ya kusikia shuhuda nyingi kutoka kwake kuwa katika madhabahu hii ambayo ipo chini ya Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kuna uponyaji. 



Kwa muda wa miaka mitano nimekuwa nikisumbuliwa na kidonda. Nimekuja hapa nikiwa na imani ya kupokea uponya baada ya kufanyiwa maombi. Naamini Mungu ataniponya tu kwani yeye ndiye mponyaji wetu. Ndugu zangu kidonda kinanitesa sana, Napata maumivu makali sana kwa kipindi chote cha miaka miatano. Maisha yangu yamekuwa ni maisha ya uchungu kutokana na maumivu makali.



Baada ya kumaliza kushuhudia, Mch. manumbu na Mch. Prisca Charles pamoja na kanisa zima waliweza kumuombea na kuvunja nguvu za giza zilizokuwa zikimtesa na kusababisha kutokea tatizo la ugonjwa wa kidonda sugu. Wakati wakimuombea aliweza kuangushwa chini huku mapepo yakipiga kelele yakitaka kutoka kwasababu yalikuwa yakiunguzwa na moto wa Yesu Krist0. Tuzidi kumuombea huyu ndugu yetu ili apokee uponyaji wake kutoka kwa Mungu.


Comments