28.10.2018: MUUMINI AJITOLEA KUKU KUCHANGIA KONGAMANO LA SHILO TANZANIA 2018

Nilibarikiwa sana siku ya Jumapili 28.10.2018 katika ibada ya Maombi ya hatari nilipoona mshirika wa Malima wa Moto Mikocheni "B" akimtoa kuku kama mchango wake kwaajili ya ujio wa kongamano la Shilo Tanzania ambalo litaanza rasmi tarehe 02 hadi 09/12/2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" Hakika mshirika huyu ana moyo wa ajabu sana na anaupendo wa dhati. Tuzidi kumuombea ili Mungu amuongezee pale alipotoa. Kama huna moyo wa hila naomba utamke jambo lolote lile kwa muumini huyu ili Mungu ambariki zaidi. Yawezekana na wewe ungetamani kuchukua baraka kutoka kwa Mungu kwa kuchangia kongamano la Shilo Tanzania 2018, basi unaweza kutuma mchango wako kwa namba hii Tigo pesa 0677 045 504. Mungu akubariki sana

---------------
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.
Mlima wa Moto Mikocheni "B"














Comments