28.10.2018: APONA KIZUNGUZUNGU KILICHOMSUMBUA KWA MUDA MREFU.

Mama huyu baada ya kuteseka kwa muda mrefu na kizunguzungu aliweza kufika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” siku ya Jumapili 28.10.2018 na kuhudhuria ibada ya Maombi ya Hatari. Mchungaji aliweza kumuombea na kupokea uponyaji wake, na hivi ndivyo alivyoshuhudia.



BWANA apewe sifa. Ninamshukuru Mungu kwa kuniponya. Wakati maombi yanaendelea, kuna mchungaji akasema “Mapepo ya uchawi yatoke”, niliona kitu kimeshuka kichwani, nikajisikia kizungzungu kikali sana, nikaona kama kuna watu wanakimbia na baadae fahamu zangu zikarudi. Ninamshukuru Mungu sana kwasababu nimepokea uponyaji siku ya leo ya Jumapili ya 28.10.2018.



Comments