21.10. 2018 | WATU WAZIDI KUFUNGULIWA KATIKA IBADA YA KUPOKEA BARAKA

Ilikuwa ni siku ya Jumapili 21.10.2018 ambapo tulishuhudia watu wakifunguliwa kutoka katika vifungo vya shetani kwenye ibada ya "KUPOKEA BARAKA" iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".






Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kuwakomboa watu wake kutoka katika mateso yaliyokuwa yakiwasumbua kwa maika mingi.



Katika kipindi cha maombi na maombezi wachungaji, wainjilisti na viongozi mbalimbali waliingia vitani kupambana na shetani ili awaachie watoto wa Mungu. Tunamshukuru Mungu katika vita hivi BWANA alijichukulia utukufu kwa kushinda vita. Watu wengi sana walitokwa na mapepo, majini na nguvu za giza zilizokuwa kikwazo katika maisha yao. Tulishuhudia mapepo yakipiga kelele na kuwagalagaza watu huku yakilalamika kuondoka. Hakika Mungu wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" anajibu kwa moto ulao.



Yawezekana unasumbuliwa na mapepo, majini, nguvu za giza zilizosababisha usio/kuolewa, usizae, usipate kazi, usipate kibali, usipate wateja wengi, usipate pesa, usitamani kusoma Neno la Mungu, umejiingiza katika ukahaba, uasherati, uzinsi, ulamaya, uongo, utapeli, ulafi, uongo, huwasaidii wazazi wako, magonjwa sugu yanakutesa, huapati promosheni kazini kwako, jamii hakuthamini tena, huaminiki, nyota yako imekufa, kila unachofanya hakifanikiwi, kazi unayofanya haiendani na kipato unachopata, unachanjwa chale, unaota ndoto mbaya, unaamka asubuhi umechoka, wachawi wanakuchezea, umekuwa ni mtu wa hasira na mambo mabaya kama hayo. Ninakuomba usikose ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Watumishi wa Mungu tutakuombea, tutakemea mapepo, tutavunja maagano ya mamabu zako, tutavunja kila kazi za shetani, tutaharibu mipango ya shetani na hatimaye tutamuita Mungu awe mlinzi wa maisha yako, kazi yako, afya yako, kazi yako, familia yako, biashara zako n.k.



Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3





































Comments