11.11.2018: WATU WAZIDI KUTOA MICHANGO YAO KWAAJILI YA KONGAMANO LA SHILO TANZANIA 2018

Naona watu bado wana hamu ya kufikia siku ya kongamano la Shilo Tanzania 2018 litakaloanza tarehe 02 hadi 9/2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Bado watu hawajachoka kutoa michango yao kwa moyo upendo kwaajili ya kufanikisha kongamano hili ambalo hufanyika mara moja tu kwa mwaka na hukusanya watu kutoka mataifa mbalimbali kwaajili ya kupokea baraka na miujiza ya SHILO. Kusanyiko hili ni kusanyiko la watu wa Mungu wote bila ya kuangalia dini ya mtu, jinsia ya mtu, kabila la mtu, taifa la mtu, umaarufu wa mtu, rangi ya mtu, viwango vya mapato ya mtu, hili ni kongamano la kila mtu.


Siku ya Jumapili 11.11.2018 katika ibada ya "KUFUNGULIWA" watu wengi sana walijitokeza katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni " wakiwa na bahasha zao kwaajili ya kuchangia kongamano hili la SHILO TANZANIA. Fedha na mali zao ndizo zitasaidia kulipia umeme, wafanyakazi watakaokuwa nasi kwa siku 8, malazi kwa wachungaji na wageni, bili za maji, kununua vifaa vya maandalizi, chakula, kuwasafirisha watu kutoka katika vituo vyao na kuwaleta kanisani kwa siku 8 na kuwarudisha, malazi kwa watu wanaotoka mikoani n.k. Kwahiyo tunahitaji sana mchango wako.


Watu hawa wanaonyesha ni jinsi gani wanampenda Mungu kwa kujinyima kununua mahitaji yao na kuamua kumtolea Mungu fedha na mali zao ili watu waokokolewe na zaidi wao wenye wapokee baraka za Mungu.


Bado nafasi unayo wewe ambaye hujatoa mchango wako, hata kama uko mikoani unayo nafasi ya kutoa kupitia TIGO PESA 0677 845 504 . Unaweza kutuma kuanzia Tshs. 100 hadi mabilioni kutoaka na jinsi Mungu alivyokubariki. Kongamano hili linahitaji sana pesa kwaajili ya kulipia mambo mbalimbali na kila jambo linahitaji pesa. Mchango wako utatusaidia sana kuhakikisha kazi ya Mungu inasonga mbele.


Utakapotuma pesa yako tunaomba jina lako lako na andika mahitaji yako na jopo la wachungaji watakuombea.


Mungu akubariki sana na tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii ambayo itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B".


Mwanangu naomba unisaidie mama yako ku-share tangazo maana uki share linafika mbali zaidi..Mwanangu chondee


































Comments