11.11.2018: WATU WAZIDI KUOKOKA NA KUMPOKEA YESU KRISTO KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAO.

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akishirikiana na Mch. Mbunda waliwaongoza sala ya toba waongofu wapya ambao waliamua kwa hiari yao kuokoka katika ibada ya "Kufunguliwa" iliyofanyika siku ya Jumapili 11.11.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Wachungaji waliweza kuwaombea, kuvunja na kuharibu nguvu za giza zilizokuwa zikiwasumbua kwa muda mrefu. Wengi wao walifunguliwa na kuwekwa huru. Baada ya maombezi walibatizwa kwa maji mengi. Siku ya Jumatatu walianza masomo yao ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Tuzidi kuwaombea ili wasonge mbele katika maisha mapya ya wokovu.
Mch. Mbunda

Tunakualika na wewe unayetamani kuokoka siku ya Jumapili kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Huu ni wakati wako wa kumrudia Mungu kwa maana hujui lililombele yako kuanzia dakika hii. Njoo kwa Yesu uokolewe. Mungu akubariki sana wewe utakayetii agizo hili na kufika kanisani siku ya Jumapili.












































Comments