11.11.2018: WATU WAPOKEA BARAKA KUPITIA IBADA YA KUSIFU NA KUABUDU.

Mtumishi wa Mungu Enock Ntontoo siku ya Jumapili 11.11.2018 katika ibada ya "KUFUNGULIWA" iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" alitubariki sana katika kipindi cha kusifu na kuabudu. Tuliona uwepo wa Mungu katika ibada hii, watu wengi sana waliguswa na nguvu za Mungu na kujazwa Roho Mtakatifu. Ilikuwa ni ibada ya tofauti sana, watu walitokwa na machozi ya furaha kutokana na ule uwepo wa Mungu uliokuwa umetanda katika nyumba ya BWANA.


Tunasoma katika Biblia ya kuwa Mungu wetu huwepo katikati ya sifa, kwahiyo siku ya Jumapili alikuwepo katikati yetu kwasababu tulikuwa tukimuimbia na kumtukuza Yeye kutokana na matendo makuu anayofaya katika maisha yetu ya kila siku. Mungu wetu amekuwa msaada wetu na kiongozi wetu katika safari yetu ya kwenda mbingu, anatulinda na mambo mengi mabaya na kuhakikisha wanae tunashinda vita dhidi ya wabaya wetu wanaotaka kutuangamiza kwa mikuki ya moto.


Tuzidi kumuombea mtumishi wa Mungu Enock Tontoo pamoja na Praise & worship Team ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa maana wamefanyika baraka katika huduma yao ya uimbaji katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Mungu amekuwa akiwatumia kwa naman aya tofauti sana na ndio maana wanapotoa sauti zao zimekuwa na nguvu za Kimungu na watu wanapokea miujiza yao. Mungu azidi kuwatunza na kuwainua ili kazi yake isonge mbele na watu waweze kuokoka na kumrudia Mungu kupitia nyimbo zao zilizojaa upako.




Kama ulikosa ibada hii basi tunakualika katika ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.




Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3















 






Comments