11.11.2018: MCH. FUNGO KUTOKA MWANZA ALIVYOWEZA KUWAOMBEA NA KUWATABIRIA WAUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" KWENYE IBADA YA KUFUNGULIWA

Mch. Fungo kutoka kanisa la Mlima wa Moto Mwanza siku ya Jumapili 11.11.2018 aliweza kuwaombea waumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwenye ibada ya "KUFUNGULIWA." Baadhi ya watu waliweza kushuhudia jinsi Mungu alivyowaponya mara tu baada ya kuombewa na mtumishi wa Mungu Mch. Fungo. Watu walibarikiwa sana na huduma yake na waliweza kufunguliwa katika vifungo walivyofungwa na maadui zao bila ya wao kutambua. 

Wakati wa maombi tulishuhudia baadhi ya watu wakitokwa na mapepo, nguvu za giza, watu waligalagazwa chini kwasababu moto wa Yesu ulikuwa ukayauguza mapepo. 


Tunamshukuru sana Mungu kwa kumtumia mtumishi wake Mch. Fungo ambaye alifanyika baraka kwa watoto wa Mungu katika ibada ya "KUFUNGULIWA." Watu wengi waliwekwa huru kutoka katika shimo la mateso la shetani.

Yawezekana ulikosa kushiriki ibada hii, tunakualika katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Itakuwa ni Jumapili yako ya kujifunza Neno la Mungu, kuhudumiwa kiroho, kuinuliwa kiimani, kujazwa nguvu mpya kutoka kwa BWANA, kubarikiwa, kupokea muujiza wako wa kuoa/kuolewa, kupata ajira, watoto, kibali, heshima, gari, kiwanja, hamu ya kusoma Neno la Mungu n.k na BWANA ataondoa mikosi, ndoto mbaya, kutopata mimba, mimba kuharibika, magonjwa sugu, kuonewa, kukosa wateja kazini kwako na mambo mengine mabaya yatakomeshwa kwa jina la Yesu Kristo.

Unachotakiwa ni kuja ukiwa na imani isiyo ya kawaida ya kwamba BWANA atakutana na wewe. Utapata muda mzuri wa kupeleka maombi yako kwa BWANA, kutubu dhambi zako na kujifunza mengi kutoka katika madhabahu ya Mungu. Wachungaji mbalimbali wamejipanga kukuhudumia siku hiyo.

Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3































Comments