11.11.2018: MAMA MRAMBA AMSHUKURU MUNGU KUMVUSHA SALAMA KATIKA JARIBU.


Ilikuwa ni siku ya Jumapili 11.11.2018 katika ibada ya "KUFUNGULIWA" iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ambapo Mzee wa kanisa na mtumishi wa Mungu mama yetu Mramba aliweza kumshukuru Mungu kumvusha salama katika changamoto aliyokuwa akipitia katika familia yake. Anasema haikuwa kitu cha kawaida lakini Mungu alioneka akimtetea na hatimaye kumtia moyo.


Ulikuwa ni wakati mgumu sana kwake pamoja na familia yake lakini BWANA aliweza kuweka wepesi na hatimaye Jumapili liweza kumtukuza Mungu na kumshukuru kwa yale aliyomtendea.


Mama Mramba aliweza Kumshukuru Mungu, pamoja na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na jopo la wachungaji na wainjilisti wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", vijana, wahudumu, viongozi na waumini kwa ujumla 
kwa kuungana naye katika kipindi kigumualichokuwa akipitia. Pia alimshukuru sana Mungu kwa kumshika mkono na kumfariji na kumvuta machozi pale alipoona hawezi kujizuia kulia kutokana na lile lilokuwa mbele yake.


Nasi tuzidi kumuombea Mungu ili mzee wetu wa kanisa ili Mungu azidi kumtumikia Mungu na kutoongoza katika safari ya kwenda mbinguni kupitia huduma yake aliyonayo katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"


Mama Mramba ni kati ya viongozi wanaojituma katika kazi ya Mungu kupitia huduma ya Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ni mama anayehakikisha kazi ya Mungu halirudi nyuma, ni mama asiyependa kuona kazi ya Mungu inaenda kiulegevu, ni mama anayejituma kwa mali zake, akili zake kuhakiksha kazi ya Mungu inasonga mbele bila ulegevu wowote. Mchango wake umefanyika baraka kwa kanisa na watu wengi wanaokoka na kumrudia Mungu kupitia huduma yake anayofanya katika kanisa letu la Mlima wa Moto Mikocheni "B". 


Kwahiyo katika maombi yako usisahau kumuombea mtumishi wa Mungu huyu ili BWANA azidi kumuinua kimwili na kiroho ili kazi kazi ya BWANA isonge mbele.


Kama ulikosa kumfariji Mama Mramba tunakualika katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ili uweza kumfariji na kumtia moyo na utajua ni changamoto gani ilimkumba mzee wetu wa kanisa. Ibada yetu itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.


Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3




Comments