11.11.2018: HAPPY KWAYA WALIVYOMTUKUZA MUNGU SIKU YA JUMAPILI YA MAOMBI YA HATARI

Siku ya Jumapili 11.11.2018 katika ibada ya maombi ya "KUFUNGULIWA" tulibarikiwa sana na uimbaji kutoka kwa wanakwa wa Happy Kwaya ya Mlima wa Moto Mikocheni "B". Kupitia nyimbo zao tulikumbushwa, tulielimishwa, tulijifunza na tuliadibishwa. Mungu azidi kuwatunza wanakwaya hawa na kuinua karama waliyopewa na Mungu. Kupitia nyimbo zao kuna watu wanaokoka, wanakumbushwa kutenda mema na kuacha maovu, waadibishwa pale wanapomkosea Mungu na wanaburudika. Tuzidi kuwaombea ili wafanikiwe zaidi kimwili na kiroho na tuzidi kupokea baraka kupitia nyimbo zao zenye upako wa aina yake.















Comments