04.11.2018: YESU AMPONYA KANSA BAADA KUFANYIWA OPERATION ILIYOSABABISHA KUPOTEZA FAHAMU KABISA

Mzee Amanyimana mwenye asili ya Burundi na ni mzee wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” siku ya Jumapili 04.11.2018 aliweza kumshukuru Mungu kwa kumponya kansa ya tumbo, alikuwa na haya ya kusema, “BWANA Yesu apewe sifa. Nilikuwa na kansa lakini Mungu alikuwa upande wangu. 


Nakumbuka nilitoka Tanzania nikaenda kwetu Burundi nikidhani nitarudi tena Tanzania, lakini sikuweza tena kurudi Tanzania. Nikiwa Burudndi nilipimwa vipimo vyote kujua afya yangu na wakagundua nina kansa. Baada ya kufanyiwa “check up” nilirudi nyumbani na wakaniambia tarehe 24 nirudi tena hospitalini nifanyiwe “Operation”. 
Tarehe ilipofika niliongozana na mke wangu mpaka hospitalini na nilipofika pale nikaingia katika chumba cha kufanyiwa “Operation” wakanikatakata tumbo langu lote na yalikuwa matundu sita. Nililazwa hospitalini kwa siku nne (4), nakumbuka siku ya Ijumaa daktari alikuja kuangalia maendeleo yangu na baada ya kuona hali yangu ni nafuu ananimbia “Sasa ninaweza kwenda nyumbani.”
 Nilimshangaa Mungu kuona mtu niliyefanyiwa “Operation” naruhusiwa kwenda nyumbani nikiwa na siku nne tu tangia nipasuliwe tumbo. Baada ya hapo wakanipa tarehe ya kurudi hospitalini kubadilisha “bandage” waliyonifunga kwenye vidonda.

Ninamshukuru sana Mungu kwani aliweza kunipa nguvu za kwenda hospiitalini mwenyewe na kurudi nyumbani kwangu. Kitendo cha kwenda hospitalini na kurudi nyumbani nikiwa naumwa vidonda kilinishangaza sana na hata waliokuwa wanajua hali yangu walishangazwa sana, hakika Mungu ni wajabu sana, wacha tumtumikie. Jamani Mungu ni mwenye UWEZO.

Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kufika tena katika kanisa Mlima wa Moto Mikocheni “B” na kuabudu na ninyi watu wa Mungu. Nimefurahi sana kuwaona tena watu wa Mungu, ninawapenda sana na asanteni sana kwa maombi yenu yaliyosababisha nikapona kansa.

Baada ya kumaliza kumshukuru Mungu, mke wake alikuwa na haya ya kusema, “BWANA Yesu asifiwe. Ninawapenda sana wana Mlima wa Moto Mikocheni “B”. Ninafurahi sana kuwaona tena. Nakumbuka nilitoka hapa mwaka 2016 na tarehe 20 Februari 2017 nilienda nyumbani Burundi kumuona mume wangu ambaye alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wake, na ilikuwa kidogo afariki.
 Shetani alipanga mipango mibaya alitaka mimi nirudi Ulaya nilikokuwa naishi nikiwa peke yangu bila ya mume wangu, alitaka mume wangu afe kule Burundi. Namshukuru Mungu aliweza kuzuia hicho kifo na kusema, “Haiwezekani.” Unajua Mungu akisema basi amesema kwani Mungu wetu ni mwenye uwezo..

Mume wangu alizidiwa sana na akapoteza fahamu. Ninawashukuru sana watu wa Mungu waliokuwa wakija kwa zamu kumuombea mume wangu apone. Maombi ya watu wa Mungu ndiyo yaliyosababisha mume wangu kupona. Wakati watu wa Mungu wakimuombea, mume wangu alikuwa taabani sana na alikuwa hasikii lolote. Ninamshukuru sana Mungu kwa kumpa uhai tena mume wangu.


Nakumbuka kuna kipindi kuna watu waliweza kumakatia tiketi akiwa hospitalini lakini mume wangu hakuweza kujua ni kiasi gani wametumia kwaajili ya kukatia tiketi, kwahiyo hatukujua kama wale watu walimdhurumu au hawakumdhurumu kwa maana mume wangu alikuwa hana fahamu kabisa ya kutambua. 
Kipindi namuuguza mume wangu tulikutana na vikwazi vingi sana, lakini Mungu alinitetea sana na kunipa njia ya kupita. Mume wangu alikuwa akiongea lugha ya kifo, nikamwambia mume wangu, “Acha kuongea lugha ya kufa bali sema utaishi milele kwa maana una kazi nyingi za kumfanyia Mungu wetu.”


Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwani kwa kusimama katika madhabahu hii ya Mlima wa Moto Mikocheni “B” ni kwa Neema ya Mungu. Kuwepo na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare hapa kanisani ni kwa neema ya Mungu. Nakuomba mtu wa Mungu usipoteze muda na kuhangaika na ya duniani kwani ni ya kupita tu. 
Hizi pesa tunazitafuta sana lakini hazitatupeleka mbinguni na kama tunazipata hizi pesa zifanye kazi ya Mungu. Jambo linguine naomba tumuogope Mungu kwani alituumba kwa mapenzi yake anajua utakachokula, utakachovaa kwahiyo tusiwe watu wa kumuudhi Mungu wetu. Mungu awabariki sana. Amen

BONYEZA HAPA KUONA VIDEO: https://www.youtube.com/watch?v=2fCE0V6ClZ8

























Comments