04.11.2018: WAUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI WALIVYOMUABUDU MUNGU KATIKA IBADA YA MAOMBI YA VITA

KIPINDI CHA KUSIFU NA KUABUDU.

Ilikuwa ni siku ya baraka sana katika ibada ya MAOMBI YA VITA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 04.11.2018. Waumini waliingia kwenye maombi ya hatari baada ya kipindi cha kusifu na kuabudu kilichoongozwa na mtumishi wa Mungu Martha Komanya kumalizika. Mungu alionekana akishusha nguvu zake kwa kila mmoja aliyejiachia kwa Mungu. Baadhi ya watu walitokwa na mapepo na nguvu za giza hasa pale wachungaji walipoingia katika kipindi cha maombi. Ilikuwa ni ibada ilitawaliwa na uwepo wa Mungu, nguvu za Mungu, na watu wengi walijazwa Roho Mtakatifu.

Kupitia maombi haya tunaamini kuna watu watakwenda kupokea miujiza yao ya kazi, kibali, safari za Ulaya, kununua viwanja, kujenga, kuzaa watoto, kusomesha watoto, kupata pesa, kulipa kodi za nyumba na ada za shule, kuponywa, kupata wateja, kuwekwa huru kutoka katika nguvu za giza na mambo mengine kama hayo.

Kama kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" tunasubiri kusikia shuhuda mbalimbali kutokana na maombi yaliyofanyika katika hekalu lwa BWANA.

Yawezekana ulikosa maombi haya na ungetamani na wewe kuombewa ili uwekwe huru kutoka katika shimo la mateso. Tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi





















Comments