04.11.2018: WATU WAZIDI KUTOA BIDHAA ZAO NA MIFUGO YAO KUCHANGIA KONGAMANO YA SHILO 2018.

Waumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na wadau mbalimbali siku ya Jumapili 04.11.2018 katika ibada ya "Maombi Ya Vita" waliweza kutoa baadhi ya mali zao na mifugo yao kwaajili ya kuchangia Kongamano Kubwa kabisa la Shilo Tanzania 2018 ambalo hufanyika mara moja tu kwa mwaka. Kongamano hili hukusanya watu kutoka mataifa mbalimbali bila ya kuchagua dini ya mtu, kabila ya mtu, rangi ya mtu, jinsia ya mtu, taifa la mtu, umaarufu wa mtu, hali ya mtu, ni kongamano kubwa kwaajili ya mataifa yote duniani na kwaajili ya watu wote bila kubagua. 


Wahubiri kutoka Tanzania na nje ya Tanzania hukusanyika pamoja kwaajili kuwaombea watu, kuwabariki, kuwafundisha Neno la Mungu, kuwakumbusha maagizo ya Mungu, kukemea na kuharibu kazi za shetani zinazowatesa watu, kuwaongoza sala ya toba kwa wale wanaohitaji kuokoka. 


Hili ni kongamano kubwa sana ambapo watu hupokea miujiza yao ya kupata watoto, wasioshika mimba kushika mimba, wasio zaa kuzaa watoto, wasio kuwa na kibali kupata kibali, ambao hawajawahi kusafiri safari nje ya nchi yao Mungu hufungua safari za nje, wasiopendelewa kupendelewa, wasio jenga kuanza ujezi, wasio na viwanja kupata viwanja, waliorudi nyuma kihuduma kuinuliwa huduma zao, wasiotamani kusoma Neno la Mungu kuhuhishwa kusoma Neno la Mungu na mambo mengine kama hayo. 


Pia huwa ni kipindi kizuri kwa watu kufunguliwa kutoka katika ndimbwi la mateso kama vile kuota ndoto mbaya, kupagawa mapepo na majini, kuchanjwa chale na wachawi, kuachwa, kufukuzwa kazi, kutopata wateja, kudaiwa madeni, magonjwa sugu , kukosa hamu ya kusoma Neno la Mungu, kutoielewa Biblia, kusengenywa, kutengwa, kutupiwa roho chafu za uzinzi, umalaya, uasherati, ushoga, ulevi, uongo, utapeli, ulafi, uongo, unyimi na mambo mengine mabaya kama hayo.


Mungu huingilia kati na kuwafungua watu kutoka katika mateso yao. Kwahiyo kwa kuona hivyo, waumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na wadau wakaona ni vyema kufanya jinsi wawezavyo kuweza kufanikisha kongamano hili la Shilo Tanzania kwa kutoa mali zao ili ziuzwe na pesa zipatikane kwaajili ya kufanikisha kazi ya Mungu na kuwaokoa wale wenye uhitaji wa kuokoka.


Kupitia kongamano hili watu wengi sana hushuhudia miujiza waliyotendewa baada na kabla ya kongamano kumalizika. Tunamshukuru Mungu kwasababu watu wengi wamekuwa wakipokea baraka zao na miujiza yao kutoka kwa BWANA baada na kabla ya kuhitimshwa kwa kongamano hili.


Yawezekana unatamani kuchangia kongamano hiili la Shilo. Unaweza kutuma mchango wako kwa TIGO PESA 0677 045 504 na Mungu atakubariki sana.


Kongamano la Shilo litafanyika kuanzia tarehe 02 hadi 09/12/2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Siku za Jumapili litaanza saa 3 asubuhi na siku za katikati ya wiki litaanza saa 9 alasiri kwa siku zote 8.


Nikualike katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3

















Comments