04.11.2018: REBECA MWENYE WATOTO NA WAJUKUU AVISHWA PETE YA UCHUMBA NA MCH. STEPHANO MGANGA

Rebeca mwenye watoto na wajukuu ambaye kwa bahati mbaya mume wake wa ndoa alifariki, Mungu aliweza kumpa mume mwema Mch. Stephano Mganga ambaye na yeye mke wake alifariki. Siku ya Jumapili 04.11.2018 katika ibada ya MAOMBI YA VITA, mtumishi wa Mungu ambaye ni muumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" mama yetu Rebeca aliweza kuvishwa pete ya uchumba na mume wake mtarajiwa Mch. Stephano Mganga katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B".
Ilikuwa ni sku ya furaha sana kwa kanisa na hasa kwa Umoja wa Wamama ambao ni "Singles" wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" chini ya kiongozi wao mzee wa kanisa dada Janeth Urasa kwa kuona mwenzao amepata mume wa kuishi naye na ni mchungaji. Kanisa lilifurahi sana na likamtukuza Mungu kwa tukio hili takatifu.


Naomba nikutie moyo wewe mama mjane ya kuwa upo uwezekano mkubwa wa kuolewa tena, usikate tamaa, endelea kupiga magoti na kuomba ili Mungu akupe mtu sahihi wa kuishi naye. Na wewe baba ambaye umefiwa na mke wako na unahitaji mke wa kuishi naye, usiache kuomba na kumtumikia Mungu kwa uaminifu. Ipo siku yako Mungu atafuta machozi yako na utapata yule umpendae kama yule uliyekuwa unampenda na Mungu akampenda zaidi.


Mungu atarejesha furaha yako ya awali, atafuta machozi yako, atakupa kicheko kwahiyo usiache kumtukia na kutenda yaliyo mema mbele zake na mbele za wanadamu.


Niongee na wewe ambaye unapitia changamoto ya kutoolewa wala kuoa baada ya kufiwa na mume wako au mke wako kipenzi. Ninakuomba ufike katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ukutane na watumishi wa Mungu ambayo wamejaa nguvu za Mungu, nao watakuombea. Mungu atafungua pazia liliziba macho yako usipate kuona mke wako mzuri au mume wako mzuri, Mungu atakupa yule uliyekuwa unangoja baada ya kifo cha yule uliyekuwa ukimpenda zaidi.


Mungu ameachia kibali katika kanisa hili la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa wale wote waliochelewa kuoa/kuolewa, walishindwa kupata wake/waume wakuishi nao baada ya kufiwa na wale waliokuwa wakiwapenda, wale wanatamani kuolewa/kuoa. 

Kuna neema ya tofauti ndani ya kanisa hili, kwahiyo nakuomba uendelee kuhudhuria ibada zetu za katikati ya wiki na siku za Jumapili ambapo ibada huanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Mungu akubariki sana. Sasa naomba UBONYEZE HAPA KUONA VIDEO YAKE: https://www.youtube.com/watch?v=8jmWuaMcsLM


















Comments