04.11.2018: MCH. SYLAVANUS KOMBA AHUBIRI JUU YA UTENDAJI KAZI KATIKA KANISA

Katika ibada ya MAOMBI YA VITA iliyofanyika siku ya Jumapili 04.11.2018 ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" tulikuwa na somo zuri sana kutoka kwa mtumishi wa Mungu Mch. Sylavanus Komba wa kanisa la Mlima wa Moto Dodoma juu ya UTENDAJI KAZI. Na hivi ndivyo alivyohubiri.


Bwana apewe sifa. Nakumbuka Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alitangaza kuwa ameanza kanisa jipya la Mlima wa Moto na sio lile kanisa la zamani tulilolizoea. Kwahiyo utendaje wetu uwe tofauti, bidii yetu ya kazi iwe tofauti, tabia yetu ya kiroho iwe tofauti. Tumekuwa tukisikia nyimbo nyingi kutoka Happy Kwaya na Joybringers Kwaya zikituhimiza kumtumikia BWANA.


TUPO KATIKA NYAKATI ZA MWISHO
Watu wa Mungu, tupo katika nyakati za mwisho na shetani anatumia nguvu zake kubwa kuharibu kanisani, kwahiyo kama kanisa linatakiwa kujiandaa kumalizia kipindi cha kumtumikia MUngu kwa mbinu zinazoendana na wakati huu tulionao.


SISI NI WATENDA KAZI WA MUNGU.
Tunatakiwa kutambua kuwa sisi ni watenda kazi katika nyumba ya BWANA. Mungu wetu ametuweka hapa kuletea mavuno na sio kitu kingine. BWANA anataka nyumba yake ijae watu. Tunaona Ibrahimu wakati Rutu na mali na kila kitu kimetekwa akawaita vijana na akawavika silaha, akawapa ujuzi namna ya kuwarudisha waliotekwa kwa BWANA na alifanikiwa.


Sisi hapa katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” kwa wiki nzima tumekuwa hapa kanisani na mbeba maono Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akitufundisha mbinu mbalimbali za kuendelea kumletea BWANA matunda. 


Ninamshukuru Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alivyokuwa mstari wa mbele katika darasa hili pamoja na wachungaji, wazee wa kanisa, wainjilisti, mashemasi, wahudumu, vijana, viongozi wa idara na washirika ambao hawakuchoka kwa wiki nzima kuwepo kwenye darasa hili la kujifunza kuhusu utendaji kazi. Tunatakiwa kutambua kuwa tunapojifunza jambo lolote mwisho wake ni lazima tufanye kazi.


NENDA UKAHUBIRI HABARI NJEMA KWA MATAIFA WAOKOKE
Marko 16:15-18. Kama watoto wa Mungu lazima tuondoke twende tukamzalie BWANA matunda, twende tukawahubirie watu. 


Kuwahubiri watu Habari Njema sio lazima ujue mistari ya Biblia, sio lazima ujue kitabu cha Mathayo mpaka Ufunuo . Tunaona Yohana aliwaambia wanafunzi wake, “Tazama wana kondoo”, Biblia inasema alipomaliza kusema, “Tazama” watu wawili walimfuata Yesu. Ndugu yake Simoni alikwenda kumwambia Simoni Petro kuwa “Tumemuona Yesu kwa Filipo”, Yesu alipomuita. Ukisoma ile sura utakuta kuna maongezeko ya watu wengi kwasababu ya kusema, “Tumemuona Yesu.” Hawa watu waliokuwa wakisema hayo maneno hawakusoma sura yoyote, hawakufunga tatu kavu. 
Tumeona baadhi ya watu wanaoenda milimani kutafuta upako kwaajili ya Uinjilisti ili wapate watu wamrudie Mungu, lakini kitu wanachokifanya ni neema ileile ambayo watu wa sasa wanatumia kwenye vikoba kutafuta wateja wao. Watu wanaotafuta wateja utaona wanasambaza habari na kusema “Hapa Tunakopesha hela kwa riba ndogo.” Natamani sasa kama Mkristo utumie moyo ule ule wa vikoba kumzalia BWANA matunda.


KITU UNACHOJIFUNZA NI LAZIMA UKIFANYIE KAZI.
Haina maana kuona mtu unajifunza jambo halafu hulifanyii kazi, Unapojifunza jambo lifanyie kazi, na sisi tumejifunza mambo mengi ya utendaji wa kazi katika nyumba ya BWANA kwahiyo tunatakiwa sasa kwenda vitani kuyafanyia kazi. Kuna watu wengi sana mitaani wanahangaika, wanateseka. Watu wengi sana katika maisha ya sasa hawahangaiki na maisha ya watu wengine. Tunatakiwa kuwa na huruma na Yule ambaye tunaona anaenda jehanamu kutokana na matendo yake mabaya.

Tunatakiwa kwenda mitaani na kuwaambia watu kuwa kuna msaada wa Mungu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B”, tuwahubirie watu kuwa kuna kusamhewa dhambi, kunakuinuliwa, kuna kubarikiwa, kuna uponya nyumbani mwa BWANA Mlima wa Moto Mikocheni “B”.


Tumeona watu wanatoka Arusha wanakuja katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” na wanapokea majibu yao. Watu hawa kuna mahali walisikia habari za Mlima wa Moto Mikocheni “B” na ndio maana walifunga safari mpaka hapa kanisani.


Ukisoma katika Biblia utakuta Yule mwanamke mwenye kutokwa damu miaka 12, Biblia inasema, “Alisikia.” Kwahiyo huwezi kusikia kama hakuna anayesema. Shida ya leo watu wengi tumevaa Ukristo na hatutaki kuwa watenda kazi, mtu akiokoka na akakaa siku mbili tatu kanisani basi ameshakuwa “boss” wa mwisho kuingia kanisani wa kwanza kutoka kanisani baada ya ibada.


KAMA HUFANYI KAZI YA BWANA UTAONDOLEWA TU
Biblia inasema, mti usiozaa utakatwa. Kuna changamoto nyingi tunapitia katika maisha yaetu kwasababu tumekataa agizo kuu kutoka kwa BWANA na agizo kuu ni kwamba tuwambie watu kuwa kwa Yesu kuna msamaha, uzima, wokovu. 

Kama watumishi wa Mungu tunapata changamoto nyingi za kiutumishi kama hatutumiki. Madakatari hutuambia kama hufanyi mazoezi mwili utakuletea shida kwahiyo ni lazima ukimbie, lazima uwe unafanya kitu na mwili una roho pia kwahiyo kama hufanyi lolote ni lazima kuwa wa kwanza kukwazika. Utakuta mtu umekaa kwenye wokovu miaka 20 lakini kitu kidogo kikikukwaza unarudi nyuma.


Inashangaza kuona kuna mtu unamwamini kabisa kuwa huyu ni mtu wa Mungu, inaimba, anaomba anaongoza mambo mbalimbali lakini akikanyagwa kidogo utasikia, “Mimi ninabaki nyumbani, siji tena kanisani”, mimi ninasema “Huu ni utoto” SOMA SEHEMU YA PILI.


BONYEZA HAPA KUONA VIDEO YAKE: https://www.youtube.com/watch?v=nQqTweG-eeM&feature=youtu.be





Comments