04.11.2018: BAADHI YA WATU WALIOKOKATIKA IBADA YA MAOMBI YA VITA

Baadhi ya waongofu wapywa waliamua kumrudia Mungu wao kwa kuokoka na kutubu makosa yao mbele ya madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 04.11.2018 katika ibada ya "MAOMBI YA VITA.". Wachungaji waliweza kuwaongoza sala ya toba na kuwaombea. Baada ya kuombewa walibatizwa kwa maji mengi. Wakati wakibatizwa wengi wao walitokwa na nguvu za giza, mapepo na majini yaliyokuwa yakipiga kelele yakitaka kutoka wakati watumishi wa Mungu wakikemea na kuharibu kazi za shetani.


Baada ya kubatizwa walingia darasani siku ya Jumatattu kuanza masomo yao ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Siku ya Jumanne ilikuwa ndio hitimisho lao la kujifunza masomo hayo.


Tunachokiomba kwako wewe uliyeokoka na kubatizwa ni kuendelea kumtafuta Mungu kwa bidii kwa kushiriki ibada, kusoma sana Biblia na kuielewa, kufunga na kuomba, kujituma katika kazi za Mungu mitaani kwako unakoishi na kanisani kwako, kuwapenda watu kama Yesu alivyotupenda sisi, kutenda yaliyomema kwa kila mtu bila ubaguzi wowote, kutangaza Habari Njema za Mungu, kuwaleta watu kanisani ili nao waokoke kama wewe, kuachana na tabia mbaya waliyokuwa mkiifanya kabla ya kuokoka, kuzishika amri kumi na za Mungu na kuzifanyia kazi katika maisha yako ya kila siku, kutenga muda wa kumsifu Mungu kwa kuimba na kucheza kwa maana Mungu wetu hukaa katikati ya sifa na mengine kama hayo.


Sasa basi, baada ya wokovu huu waongofu wapya wategemee kupokea baraka za Mungu kama watutakuwa watii na waminifu mbele za Mungu. BWANA atafungua milango ya kazi, kibali, kupata watoto, kujenga, kununua viwanja, kusomesha, kufaulu masomo yao, kupata ada za shule, kupata kodi ya nyumba, kupata marafiki watakaowasaidia katika kazi zao, wasiopata mimba watazaa, watapata afya njema na mambo mengine kama hayo.


Sisi tuliyeokoka muda mrefu, tuzidi kuwaombea hawa waongofu wapya, tuwafundishe Neno la Mungu, tuwasaidie pale wanapokwama kimwili na kiroho, tuwaonyeshe upendo wa Yesu, tuwatia moyo pale tunapoona wanaanguka kiimani, tuwatembelee na kuwajulia hali na kujua maendeleo yao ya wokovu, tuwapigie simu na kuwakumbusha kuja kanisani na mambo mengine kama hayo.


Yawezekana na wewe unatamani kuokoka kwa maana maisha yetu ya kuishi hapa duniani ni mafupi sana. Tunakualika katika ibada ya Jumapili hii ambayo itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.




























































Comments