16.09.2018: WATU WATOLEWA MAPEPO NA MAJINI KATIKA IBADA YA MAOMBI YA KUVUNJA ROHO YA UTSA NA LAANA




Jamani kuna watu wanateseka na mapepo na nguvu za giza, wanahitaji sana maombi yako. Watu hawa hawapendi kuishi maisha kama haya, wanatamani kuishi maisha ya amani na yenye furaha. Kama wakristo tunahitaji kusimama imara kumpinga shetani kwa maombi. Ndugu zetu hawa wanahitaji UHURU katika maisha yao. 






Kila unapofanya maombi yako, wakumbuke kuwaombea hawa ndugu zetu na wengine ambao wako majumbani mwetu ili wafunguliwe katika vifungo vya shetani. Kuna watu wametupiwa majini na mapepo na watu wengi kutokana na sababu mbalimbali, wengine wamelogwa kutokana na sababu mbalibali kwahiyo watu hawa wanahitaji sana msaada wako kupitia maombi. Inaumiza sana kuona mtu unashindwa kufikia malengo yako kwa kusumbuliwa na mapepo. 




Kuna watu wengine wanasumbuliwa na mapepo kutokana na wao wenyewe kuwa mbali na Mungu na kuruhusu shetani kupenya na kuingia katika maisha yao, na wengine kutokana na tamaa za kidunia wanaamua kwenda kwa waganga wa kienyeji ili wapate kile wanachokihitaji na wanajikuta wanaingia katika maagano mabaya ambayo baadae yanaanza kuharibu maisha yao. kwahiyo kama wewe ni mmojawapo watu walioingia katika maagano na shetani, ni wakati wako wa kutubu na kuungama dhambi zako na ujikabidhi mikononi mwa BWANA kuanzia sasa. Mungu anakupenda na anatamani kuanzia sasa akuokoe kama utamkubali na kuambatana naye katika maisha yako.



Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kuwafungua watu wenye mapepo siku ya Jumapili 16.09.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto MIkocheni "B" kwenye ibada ya KUVUNJA ROHO ZA UTASA NA LAANA . Watumishi wa Mungu tuliingia kazini na kuanza kusambaratisha kazi za shetani kwa kukemea kila aina ya nguvu za giza zinazowatesa watu wa Mungu. Watu wengi sana walitokwa na mapepo, majini na nguvu za giza baada ya moto wa Yesu kuunguza kila kitui kilichokuwa kikiwatesa watu hawa.



Tunakushukuru wewe uliyehusika kuwaomba watu hawa. Maombi yako yamefanyika msaada katika kuokoa maisha ya ndugu zetu hawa. Usiache kuwaombea hata unapokuwa nyumbani kwako au kazini kwako ili wazidi kufunguliwa.


Yawezekana na wewe ni miongoni mwa watu wanasumbuliwa na mapepo. Tunakualika katika ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana ili uweze kuombewa na watumishi wa Mungu. 



Utakapokanyaga katika hema la BWANA, amaini kuondoka na uponyaji wako kutoka kwa Yesu Kristo. Tumeshuhudia watu wakiingia kanisani wakiwa na mapepo lakini baada ya maombezi wanafunguliwa na kuwa huru kabisa. Amini safari hii unakwenda kufunguliwa kwa jina la Yesu.




Utakapokuwa kanisani, jiachie kwa Yesu na amaini kile unachotamkiwa na watumishi wa Mungu. Imani yako ndio itakayokuweka huru kutoka katika shimo la mateso. Yesu anaweza mambo yote, hata unalopitia Yesu anaweza kufanya kama utatii sauti yake na kufuata maagizo yake kupitia neno lake linalopatikana katika Biblia.




















Comments