16.09.2018: MTANGAZAJI WA PRAISE POWER RADIO 99.3FM BONY MAGUPA AMSHUKURU MUNGU KWA KUMUOKOA KATIKA AJALI YA GARI

Mtangazaji wa Praise Power Radio 99.3FM Bony Magupa akiwa na mke wake Jesca Honore siku ya Jumapili 16.09.2018 katika ibada ya KUVUNJA ROHO YA UTASA NA LAANA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" aliweza kumshukuru Mungu kwa kumuokoa na ajali mbaya ya gari iliyotokea katika eneo la Salenda Bridge jijini Dar es Salaam. Bony Magupa akiongea katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" alikuwa na haya ya ksema.


Bwana apewe sifa. Ilikuwa ni tarehe 04.09.2018 maeneo ya Salenda Bridge ambapo gari yangu iligongwa na kuwa nyang'anyang'a. Nakumbuka nilikuwa nimesimama kwenye foleni baada ya kusimamishwa na "trafic", wakati nimesimama, nyuma yangu nikaona gari aina ya Prado kupitia "site mirror" ya gari yangu ikiwa inakuja kwa mwendo kasi sana. Nilichokifanya ni kushikiria usukani kwani na kusubiri tukio kutokea, kwani nilikuwa sina mahali pa kwenda wakati huo kwasababu mbele yangu kulikuwa na magari mengi yamesimamishwa na "trafic". Kwahiyo ile Prado ikanigonga nyuma na mimi nikagonga gari lililokuwa mbele yangu na yale yalikuwa mbele yangu nayo yakagogwa (yalikuwa magari matano yaliyoharibika sana). Gari langu liliumia sana lakini mimi nilitoka salama bila ya kuumia popote katika mwili wangu.


Mwisho napenda kumshukuru sana Mungu, pia napenda kumshukuru sana mke wangu Jesca Honore BM na familia yangu. Mke wangu alikuwa bega kwa bega na mimi kwa maombi, na ni mke ninayempenda saa na ni ke alkiyesoma sana na anajua sana Kiingereza kwani kwake kimelala. Amesoma shule za Bishop Dr. Gertrude Rwakatare za St. Mary's.


Nawashukuru sana marafiki, wadau, wafanyakazi wenzangu wa Praise Power radio 99.3 FM, wachungaji 12 wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na bila kumuacha mama yangu kipenzi Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa maombi yao. Mungu awabariki sana.Amen.


Baada ya Bony Magupa kumaliza kumshukuru Mungu, mke wake Jesca Honore alikuwa na haya ya ksema; "Bwana Yesu Asifiwe. Namshukuru Mungu kuwepo katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" nikiwa na mume wangu akiwa ni mzima baada ya kupata ajali mbaya ya gari.


Naweza kusema ni Mungu mwenyewe aliyemponya. Nakumbuka kabla ya ajali kutokea, mume wangu aliniambia kuwa alikuwa ana-"sense" kitu kinaenda kutokea ambacho ni kibada, na mimi nilikuwa na hisi hivyo hivyo, kwani Roho Mtakatifu alikuwa ananishuhudia ndani yangu kuwa kuna kitu kibaya kinaenda kutokea. Baada ya hapo tukaingia katika maombi. Ninamshukuru Mungu kwani yale maombi tuliyoomba aliweza kuyasikia na kupinga roho ya mauti. Kwasababu kutokana ile ajali mume wangu alitakiwa asiwepo duniani, lakini ninamshukuru Mungu kwani yeye ndiye aliyeachilia ile ajali ili itokee ili jume wangu atoke salama na ajue aliyemponya na ajali ni Mungu mwenyewe.




Wakati mwingine Mungu anaachilia matukio yatokee katika maisha yako na sio kwamba ni kwasababu hana mpango na wewe bali anataka ujue ya kwamba ni Mungu mwenyewe amefanya na sio akili yako ambayo imekufanya utoke katika jaribu lako.




Kwahiyo nilipopata habari za ajali ya mume wangu nilijua ni Mungu ametenda na kumuonyesha ya kwamba mambo mazuri na makubwa yanakuja katika familia yetu. Mungu awabariki sana..Amen.




Baada ya Jesca Honore kumaliza kumshukuru Mungu, Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alikuwa na haya ya kusema. "Bwana apewe sifa. Je, Mnakumbuka Jesca Honore alikuwa ni mshindi wa kwanza wa mashindano ya Gospel Music Awards yaliyokuwa yanaandaliwa na kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na yalikuwa yanafanyika kila mwaka. Jesca Honore aliweza kushinda na kuweza kupata zawadi ya gari akiwa bado ni mtoto kabisa. lakini ninamshukuru Mungu ameolewa na mtumishi wa Mungu Bony Magupa na anaendelea kumtumikia BWANA. Mungu awabariki sana.










Comments