09.09.2018: MR. KISOVA ASHUHUDIA JINSI MUNGU ALIVYOMFANIKISHA KUFUNGA NDOA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 63 BAADA YA KUISHI NA MKE WAKE KWA MUDA WA MIAKA 34.

Katika ibada ya MWEZI WA TISA WA KUZAA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 09.09.2018 Mr & Mrs. Kisova walikuwa na haya ya kusema,:- Kwa jina naitwa Mr. Kisova nikiwa na mke wangu kipenzi Mrs. Kisova. Mimi ni mstaafu wa Jeshi miaka 10 iliyopita, kwahiyo nipo nyumbani nikifanya shughuli zangu ndogo ndogo na Mungu anaonekana akinitetea kila kuitwapo leo.



Namshukuru Mungu kwa kunifanikisha kufunga ndoa yangu nikiwa mtu mzima. Ndoa yangu ilifanikiwa kutokana na mahubiri, masomo ya Sunday School kutoka katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” pamoja na Kongamano la Marriage Revival Dinner Party 2018 lililofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". 


Mimi niliamua kufunga ndoa na mke wangu nikiwa mtu mzima wa miaka 63. Tunamshukuru Mungu tuliweza kufunga ndoa yetu maeneo ya Mbagala –DSM nikiwa na familia yangu. Nakumbuka wakati namuaga Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwamba naenda kufunga ndoa Mbagala, akaniuliza, “Mbona hufanyii hapa kwetu Mlima wa Moto Mikocheni “B”?” Nikamwambia, “Sikujipanga vizuri na ndio maana niliamua kufanya ndoa karibu na nyumbani.”



Nilivyopanga kuhusu ndoa yangu nilipanga ifanyikie kanisani tu baada ya hapo kila mtu aende nyumbani kwake, lakini watoto wangu na wajukuu zangu wakasema, “Hawezekana ndoa ishie kanisani, kwahiyo tutajichanga ili ndoa hii iwe ya mfano”.



Baada ya wanangu na wajukuu zangu kujichangisha, mke wangu aakanambia wanangu na wajukuu wanataka nihudhurie kikao cha harusi yetu. Mimi nikamjibu, “Waambie mimi siiji kwenye kikao.” Kwasababu niliona issue yenyewe ya ndoa sio kubwa sana. Baada ya siku tatu kufikia kikao chetu cha harusi, nikaona aibu nikaamua kwenda kwenye kikao ili niwasikilize. Ilipofika siku ya kikao nikawaambia, “Mimi nitachangia maji katoni 10 na kreta 5 za soda.



Siku ya sherehe ilipofika nilishangaa sana jinsi maandalizi yalivyokuwa makubwa. Yaani hata ningeibariki ile sherehe nikiwa mdogo, naamini haingekuwa kama ilivyokuwa siku hiyo. Ndugu zangu, jamaa zangu na majirani walishangaa sana kuona sherehe kubwa namna ile.




Kwa kweli ninamshukuru Mungu kwani ndoa yangu ilifanyika salama mpaka mwisho. Na mafanikio haya yote yanatokana na maombi na mafundisho ya mama yetu Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare yanayofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” kuanzia vipindi vya Sunday School mpaka ibada kuu. 




Ninachotaka kusema ni kwamba, unapoenda kanisani na ukapewa “Home Work” na ukafanya hiyo home work bila kugesi unaweza kufanikiwa, ila ukifanya kwa kugesi utafeli tu. Mimi nimefanya vizuri katika ndoa yangu baada ya kusikiliza mafundisho yanayotolewa katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” na ndio maana harusi yangu ilikuwa kubwa na ya mfano kwa wengine. 



Ninakushukuru sana Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare kwa kutulea kiroho na ndio maana tumekuwa mfano wa watu wa mataifa kiimani, Mungu akubariki sana



Naye Mrs. Kisova alikuwa na haya ya kusema, “Bwana apewe sifa..! Miaka yangu ni mingi, nimeishi na mume wangu kwa miaka 34”. Kwa ufupi napenda kuwashukuru sana, nimeona upendo wa wana Mlima wa Moto Mikocheni “B”, mmekuwa pamoja nasi, mmejumuika kuibariki ndoa yetu kuanzia mwanzo tukiwa kanisani mpaka mwisho tukiwa ukumbini. Nimeona zawadi zenu, Mungu awabariki sana. 


Mimi ninaabudu kanisa linguine, lakini mara nyingi sana napenda kuwa na mume wangu tukiabudu kanisa moja. Ninaamini ipo siku nitakuwa pamoja na wana Mlima wa Moto Mikocheni “B” na mume wangu.


Tangia nimebariki ndoa yangu nikiwa uzeeni, najiona ndio kwanza ninaanza upya safari ya ndoa yetu. Nakumbuka kabla ya kubariki ndoa yetu, kila mtu alikuwa akitoka kivyake, kila mtu anaenda kanisani kwake. Lakini sasa ninamini ipo siku tutakuwa tukiongozana na mume wangu katika kanisa moja. Mwisho napenda kuwashukuru sana kwa upendo wenu. Mungu awabariki sana.




Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alikuwa na haya ya kusema, “Bwana apewe sifa..! Wazungu huwa wanasema, “Birds of the same feathers fly together”. Ila mimi ninasema, kwasababu dada yangu anasali kwa mchungaji mwingine na ni kaka yangu anayenipenda sana, na huyu dada yangu ni Mtunzahazina hapo kanisani. Ninatamani kwenda kupiga magoti kwa mchungaji Yule na nimwambie chondechonde ninaomba hiyo familia iwe pamoja. 



Mimi kama Bishop wa mume wako ninakukaribisha sana Mlima wa Moto Mikocheni “B”, na Mungu akifungua milango ya kuja kusali hapa ninakukaribisha sana dada yangu. Mlima wa Moto hatuzeeki kabisa, kama unavyoona Bishop wako sizeeki.











Comments