09.09.2018: MERCY MASIKA NA MUNALOVE WALIVYOMTUKUZA MUNGU KATIKA IBADA YA MWEZI WA TISA WA KUZAA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Matukio katika picha ya watumishi wa Mungu Mercy Masika mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Kenya na Munalove mjasiriamali na mdau wa waimbaji wa nyimbo za Injili katika uandaaji wa matamsha na kuwa-support waimbaji binafsi; siku ya Jumapili 09.09.2018 waliweza kuhudumu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwenye ibada ya MWEZI WA TISA WA KUZAA. Mercy Masika aliweza kushusha uwepo wa Mungu kwa njia ya uimbaji, watu walibarikiwa sana. Munalove aliweza kuinua IMANI za watu pale aliposimulia jinsi mwanae kipenzi Patrick ambaye ni marehemu kwa sasa alivyoweza kumshauri kuokoka na kuacha na starehe za dunia na pia alivyomsihi mama yake kuondoa tattoo zake. Munalove aliweza kuukubali ushauri wa mwanae na kuweza kuokoka. Na hiivi sasa yuko katika harakati za kufuta tattoo zake. Ukitaka kujua mengi kuhusu Munalove na Mercy Masika unaweza kuingia katika Youtube Account zao na huko utajifunza mengi juu ya maisha yao.

 Mercy Masika (kushoto)  na Munalove (kulia)




































Comments