02.09.2018: WALIOBATIZWA KATIKA IBADA YA KUZAA MUUJIZA WAKO

Baadhi ya waongofu wapya waliokoka katika ibada ya "KUZAA MUUJIZA WAKO" iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 02.09.2018. Mch. Asenga na wainjilisti wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" waliwabatiza kwa maji mengi baada ya kuongozwa sala ya toba na kuombewa na Mch. Elizabeth Lucas. 

Kama Biblia inavyotuambia ya kuwa mtu akibatizwa kwa maji mengi na kumkiri BWANA wetu Yesu Kristo kuwa ni Bwana na Mwokozi wa Maisha yake, dhambi zake zinafutwa na jina lake linafutwa katika kitabu cha HUKUMU na kuandikwa katika kitabu cha UZIMA wa milele, kwahiyo watu hawa kuanzia sasa hawana dhambi mpaka watakapoamua wao wenyewe kutenda dhambi tena baada ya kubatizwa. Hivi sasa wameokoka, wamejazwa nguvu mpya kutoka kwa Mungu, wanaongozwa na Roho Mtakatifu, ni watakatifu, wamaekuwa viumbe vipya kabisa. Tuzidi kuwaombea katika safari yao mpya ya WOKOVU, kuwa karibu nao na kuwafundisha Neno la Mungu, kuwatia moyo wanapopitia majaribu, kuinua imani zao, kuwapafa faida za kumtumikia Mungu, kuwaongoza katika njia sahihi ya kwenda kwa BABA mbinguni na mambo mengine kama hayo. Kumbuka na wewe ulivyookoka kuna watu walitumia muda wao kukubatiza, kukuombea, kukuongoza katika safari ya kuelekea kwa Mungu wetu mbinguni.

Je, Wewe ambaye hujaokoka, ungetamani KUOKOA SASA? Tunakualika katika ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Tupo kwaajili ya kukuongoza sala ya toba, kukuombea, kukubatizwa na Mungu yupo tayari kufuta jina lako katika kitabu cha HUKUMU na kukuandika katika kitabu cha UZIMA.

Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3










































































Comments