02.09.2018: KIJANA MWENYE HIRISI AJISALIMISHA KWA YESU KATIKA IBADA YA KUZAA MUUJIZA WAKO



Katika ibada ya KUZAA MUUJIZA WAKO iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 02.09.2018 kwenye kipindi cha maombezi, kijana mmoja alipagawa mapepo na kuweza kutoa hirizi yake huku akihangaika kwa kugalagala chini. Watumishi wa Mungu waliweza kukemea roho chafu na baadae kuichoma hiyo hirizi.

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kumuokoa huyu kijana kutoka katika mikono ya shetani na kumuweka katika mikono salama.
Yawezekana una hirizi ambazo uliridhishwa na mama yako, baba yako, ndugu zako, babu yako, bibi yako n.k. na imekuwa ikikusumbua na umekuwa ukiwatesa watu kwa kuwaloga kwa kutumia hiyo hirizi yako. Tunakuomba uache hiyo tabia na ilete hiyo hirizi nyumbani mwa BWANA tuichome na tukutenganishe na maagano uliyoyafanya na hao waliokupa hiyo hirizi.
Mungu hapendi kuona watu wakitumia nguvu za giza kuwatesa wengine, watu wakitumia vitu kama miungu yao. Watu hawa hawatauona ufalme wa Mungu mpaka wametubu dhambi zao na kuacha tabia zao mbaya.
Maisha ni kama giza nene, hujui lililo mbele yako kuanzia sasa, unaweza kujidanganya kuwa utaiona kesho au utaleta uchawi wako uchomwe kesho. Hujui ni jambo gani liko mbele yako litakalokatisha uhai wako kabla ya kesho yako kufikia, kwahiyo linalowezekana sasa lifanye sasa usije ukafa na huo uchawi wako na ukaikosa mbingu.
Wana Mlima wa Moto tunakupenda na ndio maana Mungu ametuweka hapa kwaajili ya kuokoa maisha yako na kukuonyesha njia ya kwenda mbinguni kwa BABA. Huu sio wakati wa kumtumikia shetani au kuabudu miungu bali ni wakati wa kumrudia Mungu na kumuabudu Yeye. 
Unaweza ukajidanga na kusema ngoja nipate utajiri kwa kutumia nguvu za giza na ukashangaa huo utajiri unageuka kuwa jeneza lako na kukutenga na ufalme wa Mungu. Kuna watu matajiri sana na wanatumia nguvu za giza lakini utajiri wao unawatesa kutokana na masharti magumu waliyopewa na wachawi, wengine wanaua mama zao, watoto zao, ndugu zao, wanalala chini, wanakula mlo mmoja, wanachagua vyakula, hawavai wakapendeza, afya zao ni migogoro na mambo mengine kama hayo. Utajiri wao umegeuka kuwa adui katika maisha yao. Usione watu wana magari mazuri, majumba makubwa, pesa nyingi lakini hawana amani kutokana na maagano waliyoyafanya na waganga wao na miungu yao.

Mungu akusaidie umrudie Mungu kuanzia sasa.














Comments