02,09.2018: FAMILIA YA MZEE WA KANISA MAMA BUHATWA NA MUME WAKE WAMSHUKURU MUNGU KWA KUWAPIGANI VITA KATIKA MARIBU YAO YA KIFA

Mr. & Mrs. Buhatwa ambao ni wazee wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 09.09.2018 kwenye ibada ya MWEZI WA TISA WA KUZAA waliweza kumshukuru sana Mungu kwa kuwavusha katika mapito waliyokuwa wakipitia ya kifamilia. Mungu alikuwa upande wao kuanzia mwanzo mwa tatizo lao mpaka hatima yake.

Mr. Buhatwa alikuwa na haya ya kusema. "Kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa kutufikisha mahali hapa leo na kuweza kuja kuabudu pamoja. Tunamshukuru Mungu kwa majaribu yaliyotukua katika familia. Tunawashukuru sana kwa maombi, kwani tuliona kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" wakiwa pamoja nasi tangia jaribu litukute, na walikuwa wakija kwa nyakati mbalimbali kututia moyo na kutuombea.


Tulishuhudia miujiza ya Mungu ikitendeka wakati watu wa Mungu walivyokuwa wakituombea bila ya sisi kujua.




napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa mke wangu kwani nilikuwa naye muda wote wa matatizo yetu, alionyesha upendo wa dhati kutoka moyoni mwake, hakika nampenda sana mke wangu.


Napenda kumshukuru sana mama yetu Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare kwa kumuamini mke wangu na kuwa kiongozi wa wamama wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na pia kuwa mzee wa kanisa hili



Pia namshukuru sana Mungu kwa kumuwezesha mtoto wetu kumaliza "Degree" yake ya kwanza wa UCHUMI aliyopita China.. Kama tunavyojua mtoto akiwa nje ya nchi yako huko hakuna mjomba wala shangazi atakayesema hili afanye na hili asifanye. Kuna watu wengine wanarudi nchini kwao wakiwa hawana hata hiyo "Degree" waliyokuwa wakitafuta kwa miaka mingi, wengine wanarudi na mauzauza tofauti na yale malengo waliyokuwa wakitegemea kupata baada ya kuhitimu masomo yao; lakini mimi ninamshukuru Mungu mwanangu ameweza kupata "Degree" yake ya UCHUMI na akiwa na akili zake timamu.




Bado nazidi kumshukuru Mungu kwani binti yetu amefaulu kidato chake cha sita.




Pia napenda kumshukuru sana Mungu kwa kuwa na mama yangu ambaye ni huyu hapa. Tunaishi na mama yetu kwa amani na upendo. Mama yetu amekuwa akikupenda sana Mama yetu Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare. Leo Bishop ulihubiri kwamaba "Kuna sababu watoto kuwapenda kwasababu wamama wanatutendea mengi mazuri yasiyo na hesabu."



















Comments