02.09.2018: BISHOP MHE. DR. GERTRUDE RWAKATARE ALIVYOWAKUMBATIA NA KUWAOMBEA WAZEE WA KANISA KATIKA IBADA YA KUZAA MUUJIZA WAKO

Baadhi ya wazee wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" wakiombewa katika ibada ya KUZAA MUUJIZA WAKO iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 02.09.2018.

Je, Unahitaji kuombewa na watumishi wa Mungu waliochanguliwa na Mungu kwa kazi yake? Je, Unahitaji Uponyaji na baraka kutoka kwa Mungu kupitia watumishi wake? 

Mungu anaweza yote, hata hilo unalodhani ni gumu kwako, Mungu anaweza kulitatua na kulikokmesha lisikurudie tena. Endelea kunyenyekea mbele za Mungu na kutenda yaliyo mema mbele zake na mbele za wanadam, acha matendo yako mabaya, na mzaha katika kazi ya Mungu, usipende kuwatisha tamaa watu wanaomtafuta Mungu wala kujikatia tamaa wewe mwenyewe. Amini Ipo sekunde, dakika, saa, siku, wiki, mwezi au mwaka utaona milango yako ikifunguliwa katika ndoa yako, familia yako, biashara yako, watoto wako, uzao wako, ndugu zako, miradi yako n.k. kwasabu ulikuwa mwaminifu mbele za Mungu na mvumilivu. Hakuna aliyeomba kwa Baba na akanyimwa, bali kila unachoomba Mungu anakupa bure.

Ishi maisha ya IMANI na matumaini utaona mkono wa Mungu katika maisha yako. Unapoishia wewe kuwaza ndipo Mungu anapoanzia. Wati watumishi wa Mungu kwani Mungu ameweka baraka zako mikono mwao.

Sasa, nikualike katika ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada yetu itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.




























Comments