02.09.2018: BAADHI YA WAUMINI WALIOAMUA KUJIUNGA NA KWAYA YA JOYBRINGERS KATIKA IBADA YA KUZAA MUUJIZA WAKO

Hawa ni baadhi ya watu walioamua kujiunga na Joybringers Kwaya ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 02.09.2018 kwenye ibada ya KUZAA MUUJIZA WA MUNGU. 

Tuna kila sababu ya kukupongeza wewe uliyeamua kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. Ni maombi yetu Mungu azidi kukulinda na kukubariki kutokana na kazi ya Mungu ambayo umeamua kuifanya katika hekelu lake la Mlima wa Moto Mikocheni "B". 

Tunatambua ya kuwa Mungu wetu ni Mungu wa sifa, ni Mungu anayependa sana kuona watoto wake wakimsifu kwa nyimbo na kumwabudu kwa roho wa kweli. Kwahiyo maamuzi yako ya kumuimbia Mungu ni maamuzi sahihi na BWANA anakwenda kutukuzwa kupitia kinywa chako. Kupitia wewe, watu wataokoka, wataacha dhambi, watajifunza, wataellmishwa, wataadibishwa kupitia ujumbe utakao kuwa ukiuimba katika madhababhu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Yawezekana kuna mtu anatamani kujiunga na kwaya zetu za Mlima wa Moto Mikocheni "B" (Happy Kwaya na Joybringers Kwaya), nafasi zipo na Mwalimu yupo wa kukufundisha jinsi ya kuimba na kucheza. Mafundisho ya uimbaji yanafanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 9 alasiri.

Pia tunapenda kukualika katika ibada ya Jumapili hii ambayo itaanza saa 3 mchana hadi saa 9 alasiri.

Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3






















Comments