26.08.2018: HAPPY KWAYA NA JOYBRINGERS KWAYA WALIVOMSIFU MUNGU KATIKA IBADA YA KUPIGANIWA NA BWANA



Siku ya Jumapili 26.08.2018 kwenye ibada ya KUPIGANIWA NA BWANA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" Happy Kwaya na Joybringers Kwaya waliweza kumtukuza Mungu kwa njia ya nyimbo na kucheza ambako kulitubariki sana na kutusogeza katika uwepo wa Mungu. Ujumbe uliokuwa ukiimba umeinua imani zetu na kutupa nguvu ya kumtumikia Mungu. Nyimbo zao zenye upako zilitufanya tuweze kutafakari ukuu wa Mungu, upendo wa Mungu, huruma za Mungu, neema ya Mungu, upole wa Mungu, hekima ya Mungu na jinsi anavyotupigania katika maisha yetu wakati wa shida na raha.
Joybringers Kwaya

Waimbaji hawa wamefanyika baraka kwa kanisa na kwa Taifa letu la Tanzania kutokana na jinsi wanavyojituma katika kazi ya Mungu waki bado ni vijana kabisa. 
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Mbali na kuwa na majukumu mengi ya maisha lakini waimbaji hawa wamekuwa wakitenga muda wao kwaajili ya kufanya mazoezi ya kuimba ili siku ya Jumapili waweze kutubariki na kuinua imani zetu. Hakika tumeona matunda makubwa kupitia waimbaji hawa.


Tuzidi kuwaomba waimbaji hawa ili wasonge mbele kwa kazi ya Mungu. Tuwaombee katika masomo yao, kazi zao, familia zao, afya zao, biashara zao, huduma yao, vipaji na karama zao, uzao wao n.k ili Mungu awabariki na wazidi kusonga mbele kwaajili ya KUMSIFU MUNGU wetu aliye hai.

Mwisho, naomba nikualike katika ibada ya Jumapili hii ambayo itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Walete wenye shida mbalimbali na BWANA wetu atawasaidia.























Comments