12.08.2018: BAADHI YA WATU WALIOKOKA NA WAKIOMBEWA NA BISHOP DR.GERTRUDE RWAKATARE KATIKA IBADA YA KUFUNGULIWA KATIKA VIFUNGO VILIVYOKUZUIA KUFIKIA MALENGO YAKO

Bwana Apewe sifa. Leo nimeona ni vyema nikuletee video ya maombi ya Kufunguliwa katika Vifungo Vilivyokufunga Usifie Malengo Yako. Maombi haya yalifanyika siku ya Jumapili 12.08.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" ambapo Bishop Dr. Gertrude Rwakatare nikishirikinana na wachungaji 12 pamoja na waumini tuliweza kumuomba Mungu ili aweze kutufungua katika vifungo vilivyotufunga tusifikie yale malengo yetu. 

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu maana tuliona uwepo wa Mungu katika ile ibada ya maombi. Tulihisi kuguswa na mkono wa huruma wa mwenyezi Mungu. Na baadhi ya watu walipokea miujiza yao katika kipindi cha maombezi.

Natamani sana kuona unapata muda maalum kwaajili ya kufanya maombi. Kupitia maombi kuna majibu yako na uponyaji wako. Ipo nguvu ya Mungu katika maombi. Watu wanafunguliwa kutoka katika minyororo iliyowafunga wasifikie malengo yango. Kwahiyo jitahidi sana kutenga muda wako mzuri kwaajili ya kuongea na Mungu wako kwa kufanya maombi. Mara nyingi adui yako hupata shuda anapoona unafanya maombi ya vita dhidi yake.

Ukitaka kuiona VIDEO HII BONYEZA HAPA: https://www.youtube.com/watch?v=tOHq-sz49DI&feature=youtu.be

Na wewe ambaye ulikosa ibada hii, ninakualika katika ibada ya Jumapili hii kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3






















Comments