08.09.2018: MATUKIO KATIKA PICHA YA BISHOP DUNSTAN MABOYA AKIZINDUA SEMINA YA MID YEAR CROSS OVER 2018

Matukio katika picha ya Bishop Dunstan Maboya alipozindua rasmi semina ya MID YEAR CROSS OVER 2018 inayoendelea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Uzinduzi huu ulifanyika siku ya Jumapili 08.07.2018, kwahiyo tunakualika sana katika semina hii ya siku 8 ambayo itahitimishwa siku ya Jumapili 15.07.2018 kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Na siku ya katikati ya wiki semina inaanza saa 9:30 alasiri. Tunakualika sana katika semina hii ambayo hufanyika mara moja tu kwa mwaka na ukifika utakutana na watumishi wa Mungu Mch. Sylvanus Komba kutoka Dodoma, Bishop Dunstan Maboya, Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare na jopo la wachungaji zaidi ya 10 watakaokuombea na kukutamkia baraka kwa miezi iliyobaki kumaliza mwaka 2018. Yawezekana kuna vitu ulivipanga lakini havijatimia kwa wakati uliotarajia, basi AMINI baada ya semina hii BWANA atafanya njia pasipo na njia. Jiandae kupata somo alilolifundisha Bishop Dunstan Maboya siku ya Jumapili 08.07.2018

Usafiri wa kufika kanisani siku ya Jumapili ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3

Bishop Dunstan Maboya
















































Comments