08.07.2018: WAUMINI WALIOSHIRIKI SIKU YA KWANZA YA SEMINA YA SIKU 8 YA KUMKABIDHI MUNGU NUSU MWAKA ULIOBAKI KUFIKI 2018

TUTAFAKARI HII MISTARI INAYOELEZEA KUHUSU KUMSIFU MUNGU WETU WA MBINGUNI.

1. Pigeni vigelegele vya furaha; ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo (Zaburi 32:11b. Maneno mepesikukazia).


2. Mpigieni Bwana vigelegele, enyi wenye haki, kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. Mshukuruni BWANA kwa kinubi, kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa. Mwimbieni wimbo mpya, pigeni kwa ustadi kwa sauti ya shangwe (Zaburi 33:1-3.


3. Mpigie Mungu kelele za shangwe nchi yote; imbeni utukufu wa jina lake; tukuzeni sifa zake.Mwambieni Mungu, ‘Matendo Yako yatisha kama nini! Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako, adui zako watakuja kunyenyekea mbele zako. Nchi yote itakusujudia na kukuimbia, naam, italiimbia jina lako’ (Zaburi 66:1-4. Maneno mepesi kukazia).


Tunakushukuru sana wewe ambaye ulifika katika Ufunguzi wa semina ya siku 8 ya kumshukuru Mungu kwa kumaliza miezi sita tangia mwaka uanze na kufanya maombi ya Kumkabidhi Mungu wetu nusu mwaka uliobaki kumaliza mwaka 2018. Ulitenga muda wako na kuona ni vyema muda huu ukautumia kushiriki semina hii ambayo inajulikana kwa jina la Mid Year Cross over ambayo itaahitimishwa siku ya Jumapili 15.07.2018.


Pia tunapenda kumshukuru sana mzee wa kanisa Martha Komnaya na kikundi cha kusifu na kuabudu cha Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa jinsi walivyofanya kazi kubwa sana wakiongozwa na Roho Mtakatifu kuhakikisha watu wanabarikiwa na uimbaji, wanapokea majibu yao, wanafarijika, wanafurahia uwepo wa Mungu, wanaburudika na wanaguswa na nguvu za Mungu.


Wewe ambaye ulikosa kufika kwenye uzinduzi wa semina hii siku ya Jumapili na wewe uliyefika na kukanyaga katika kanisa la miujiza la Mlima wa Moto Mikocheni tunakualika kuungana nasi katika semina hii ambayo inanza saa 9:30 alasiri kwa siku 8 isipokuwa siku ya 8 ya `jumapili itaanza saa 3 asubuhi























Comments