08.07.2018: MZEE WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" AMSHUKURU MUNGU KUFIKIA UTU UZIMA SIKU YA UZINDUZI WA MID YEAR CROSS OVER 2018

Naataka kuongea na wewe ambaye unahisi huwezi kufanya kazi ya Mungu hekaluni mwake eti wewe ni boss, wewe ni tajiri sana, wewe ni maskini sana, wewe kiongozi mkubwa katika familia yako, wewe ni msomi sana, wewe ni mtoto wa tajiri, wewe ni mtoto wa maskini, wewe ni kijana sana, wewe ni mzee sana, wewe kiongozi mkubwa serikalini, wewe ni mlemavu, wewe ni mheshimiwa, wewe ni maarufu sana, wewe ni staa katika taifa lako n.k. BWANA anakuhitaji wewe kama wewe na sio pesa yako, utajiri wako, mali zako, umaskini wako, nafasi yako kazini, elimu yako, umaarufu wako n.k. Tunaona Yesu Kristo alianza kazi ya Mungu akiwa ni kijana mdogo ambaye ametoka katika familia ya watu wa kawaida sana, amezaliwa katika zizi la ng'ombe, mtoto wa Mungu, alikuwa maarufu sana kuliko wewe, n.k lakini hakuangalia nafasi yake wala hali yake ya kiuchumi au uhusiano wake na Mungu bali aliingia kazini kuokoa roho za watu.

Kila siku BWANa analia, anasema "Watenda kazi wake ni wachache nyumbani mwake" Kwahiyo unayo nafasi kubwa kwa kutumia karama yako, elimu yako, umaarufu wako, ustaa wako, kipaji chako n.k kufanya kazi ya Mungu. 

Unaweza kujiuliza ni kazi gani unaweza kufanya katika hekalu la BWANA?
Unachotakiwa kwanza ni kujitambua wewe una karama gani na unaweza kufanya nini katika hekalu la BWANA? Kama wewe ni mwimbaji basi unaweza kumuimbia Mungu, kama wewe ni mtangazaji unaweza kutangaza matendo makuu ya Mungu, kama wewe ni muhubiri una weza kuhubiri habari njema, kama wewe umebarikiwa kuwa na fedha nyingi unawezo kuwa ni mtu kusapoti kazi ya Mungu kwa fedha zako, kama wewe ni maarufu uanweza kutumia umaarufu wako kuleta watu kwa Yesu au kuleta watu watakasapoti huduma ya Mungu, kama wewe msomi wa kitu fulani unaweza kutumia elimu yako kwa BWANA, kama wewe ni mfugani unaweza kufuga mifugo kwaajili ya kuongeza miradi ya kanisa, kama wewe ni mkulima unaweza kutoa mazao yako kanisani na ikasaidia watu wenye uhitaji n.k.

Tuna kila sababu ya kumshukuru mzee wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa kututia moyo na kutukumbusha mengi kuhusiana na ushuhuda wake ambao uligusa umri wake, kazi yake, majaribu aliyopata kipindi anafanya kazi, mafanikio aliyoyapata akiwa kazini, miradi yake, kustaafu kazi yake na msimamo wake na Mungu baada ya kustafu kazi.

Kupitia ushuhuda huo tulijifunza kuwa haijalishi tuna umri mkubwa kiasi gani lakinii bado tuna nafasi kubwa katika kulijenga hekalu la Mungu. hajalishi tumefanikiwa kiasi gani kiuchumi lakini bado tuna nafasi kubwa sana ya kuwaleta watu kwa Yesu, hajalishi tumepitia chanagamoto kubwa kaisi gani lakini tuna nafasi kubwa ya kuwaokoa watu kutoka katika vifungo vya shetani kupitia

Haijalishi umestaafu kazi ofisini kwako lakini bado Mungu anakuhitaji kufanya kazi yake katika hekalu lake kwasababu kwa Mungu hakuna suala la kustaafu kufanya kazi ya BWANA. Kila mtu anawajibika kufanya kazi ya Mungu kulingana na uwezo wake na uzoefu wake.

Mungu anwahitaji wazee kwaajili ya kutoa maelekezo na ushauri kwa vijana ili waweze kufanya kazi ya Mungu kwa ustadi na umakini.

Pia alimshukuru sana Mungu kwa kumpigania wakati akifanya kazi serikalini. Amepitia changamoto nyingi lakini BWANA alimshika mkono na kumlinda. Akishuhudia madhabahuni alisema mbali na kuwa kiongozi katika idara aliyokuwa akifanyia kazi na kuzunguka nchi mbalimbali hakuweza kumuacha Mungu na kumtumikia Mungu kwa uaminifu. Mwisho aliahidi kutumikia Mungu kwa asilimia zote kwasababu bado ana nguvu za kufanya kazi ya Mungu.

Sasa basi, wewe ambaye hukuweza kufika katika uzinduzi wa semina ya siku 8 ya Mid Year Cross Over 2018 ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka, na mwaka huu 2018 itahitimishwa siku ya Jumapili 15.07.2018 saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"; tunakualika kushiriki semina hii ambayo ni semina ya kumshukuru Mungu kutulinda na mabaya na kutubariki katika maisha yetu ya kila siku kwa miezi sita iliyopita na kumkabidhi Mungu miezi sita iliyo mbele yetu ili azidi kutushika mkono na kutuvuta kuingia mwaka 2019. Jitahidi sana kuwahi mapema kwani semina hii inaanza saa 9:30 alasiri kila siku na siku ya Jumapili itakuwa ikianza saa 3 asubuhi. Walete wenye shida mbalimbal na YESU mtenda miujiza atawaokoa na kuwaponya.

Siku ya Jumapili usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3




















Comments