08.07.2018: MZEE WA KANISA KIWURA ALISALIMU KANISA SIKU YA UZINDUZI WA MID YEAR CROSS OVER 2018

Katika uzinduzi wa semina ya siku 8 ya Mid Year Cross Over 2018 iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 08.07.2018, mzee wa kanisa ambaye ameshawahi kuwa waziri katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Kiwura siku ya Jumapili aliweza kupata nafasi ya kuwasalimu waumini wa kanisa hilo na kuwaahidi kuwa hataliacha kanisa lake analolipenda kutokana ndani ya moyo wake. Kuna mambo mengi sana Mungu amemtendea pamoja na familia yake kupitia huduma ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" ana anatamani kuona watu wanazidi kumtumikia Mungu kupitia huduma hii ya Mlima wa Moto Mikocheni "B", kwasababu kupitia huduma hii Mungu anatoa majibu kwa kila anayemtafuta kwa bidii na watu wengi sana wamefanikiwa kiroho na kimwili kupitia huduma hii. Kwahiyo wewe unayeabudu nasi endelea kunyenyekea mbele za Mungu na kufanya kazi ya Mungu bila kuchoka. Muangalie Mungu na msikilize Mungu, uasiangalie wanadamu wala kuwasikiliza sana wanadamu wanaweza kukukatisha tamaa. Macho yako yamuangalie Mungu tu kwani yeye ndiye nguzo ya maisha yako. watii watumishi wa Mungu ili mambo yako yanyooke.


Tukualike katika semina hii ya siku 8 ambayo itahitimishwa siku ya Jumapili 15.07 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Semina hii ainaanza saa 9:30 alasiri kwa siku za katikati ya wiki na siku ya Jumapili inaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.
Mungu na akubariki sana.









Comments