08.07.2018: MESS CHENGULA APAGAWISHA WAUMINI KATIKA SEMINA YA MID YEAR CROSS OVER 2018 MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Tunapenda kumshukuru sana mtumishi wa Mungu Mess Chengula kwa nyimbo yake ambayo ilitubariki sana katika uzinduzi wa semina yetu ya MID YEAR CROSS OVER 2018 iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 08.07.2018. Nyimbo yake ilitufundisha, ilitusogeza karibu na Mungu, ilituinua, ilituadibisha, ilituburudisha kwa kiasi kikubwa sana..

Wewe ambaye hukufika siku ya Jumapili na wewe ambaye ulifika siku Jumapili, tunakualiaka tena siku ya leo katika semina hii ya siku 8 ya Mida Year Cross Over iliyoanza Jumapili tarehe 08 na itahitimishwa siku ya Jumapili 15.07.2018 hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Semina hii hufanyika mara moja tu kwa mwaka kwaajili ya kumshukuru Mungu kwa kutulinda kwa miezi sita na kumkabidhi Mungu wetu miezi sita iliyobaki kumaliza mwaka.

Hakuna anayejua kitu gani kibaya kitamkuta hapo baadae, kwahiyo ni vyema kuwa katika mikono salama ya Mungu. Kuna wabaya wako wamepanga kukumaliza kwa miezi sita hii lakini ukiwa na Mungu hakuna baya litakukuta kwa jina la Yesu Kristo. Kuna malengo yako uliyapanga yafanyike ndani ya mwaka mmoja, lakini kama hauko vizuri la Mungu ni vigumu sana kufanikisha malengo yako kwahiyo ni bora ukamkabidhi Mungu wako kupitia semina hii.

BWANA akusaidia sana kutambua umuhimu wa semina hii katika maisha yako. Tumeona watu wengi walioshiriki semina kama hii kwa miaka iliyopita wakiwa na maisha mazuri kabisa. Njoo tumlilie Mungu na kumkubusha Mungu yale maombi tuliyoomba kwa miezi sita iliyopita. Mungu akubariki sana na tuktane saa 9:30 alasiri kwa siku za katikati ya wiki na siku ya Jumapili ni saa 3 asubuhi hadi 8 mchana.

Mess Chengula na Bony Magupa (kushoto)




















Comments