08.07.2018: MCH. SYLVANUS KOMBA ANUNUA "HEADPHONE" KWAAJILI YA PRAISE POWER RADIO 99.3FM KATIKA UZINDUZI WA MID YEAR CROSS OVER 2018

"Kutoa ni Moyo". Mch. Sylvanus Komba wa kanisa la Mlima wa Moto Dodoma baada ya kuona kuna uhitaji wa "Headphone" katika kituo cha Praise Power Radio 99.3FM aliweza kutumia maarifa yake na hekima zake na kuweza kuongea na mzungu mmoja na kumpa habari za kituo cha Praise Power Radio 99.3fm na hatimaye mzungu huyo aliweza kuvutiwa na habari njema za Mchungaji na kuweza kumuuzia headphone kwa bei ya chini sana ukilinganisha na bei ya dukani. Baada ya kuzinunua alimua kuzikabidhi madhabahuni kwa BWANA Mlima wa Moto Mikocheni "B". Je, ni kitu gani unajifunza kutoka kwa Mch. Sylvanus Komba kuhusu utoaji? Unajifunza nini kutoka kwa mzungu kuhusu huruma na upendo? Unajifunza nini kwa kituo cha Praise Power radio 99.3fm kwa huduma yake mpaka watu wanajinyima kununua vitu wanavyotaka na kuamua kujitoa kununua vifaa vya radio? Unajifunza nini kwa mbeba maono wa Praise Power Radio. naamini kuna kitu umejifunza na utaenda kukifanyia kazi.

Yesu ametuagiza upendo, kwahiyo unapoona mwenzako analia njaa msaidie chakula, unapoona mwenzako analia kuhusu kazi msaidie apate kazi na baada akusaidie, unapoona mwenzako unashindwa kucheza mpira

Kumbuka, siku ya Jumapili kuliwa na uzinduzi wa Semina ya Mid Year Cross Over ambayo inaendea kila siku kuanzia saa 9: 30 alasiri na siku ya Jumapili semina inaanza saa 3 aubuhi hadi saa 8 Wote mnakaribishwa.
Kutoka kushoto ni Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare, Mch. Sylvanus Komba na Mch. Stanley Nnko











Comments