08.07.2018: MCH. MAINAH AONGOZA MAOMBI YA KUMSHURU MUNGU KUMALIZA MIEZI NA KUKABIDHI KWA MUNGU KWA MIEZI IJAYO | MID YEAR CROSS OVER

Siku ya Jumapili ya tarehe 08.07.2018 katika uzinduzi wa semina ya siku 8 ya Mid Year Cross Over iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" Mch. Baraka Mainah kutoka Kenya aliweza kutuongoza katika maombi ya kumshukuru Mungu kwa kutupigania kwa miezi sita iliyopita tangia mwaka 2018 uanze na pia alifanya maombi ya kukabidhi maisha yetu kwa Mungu kwa miezi sita ijayo ya kumaliza mwaka 2018

Semina hii inaendelea katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 9:30 alasiri kila siku na siku ya Jumapili 15.07.2018 semina hii itahitimishwa kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 9 alasiri.

Kwahiyo unayo nafasi ya kushiriki maombi haya yanayoongozwa na na mtumishi wako Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Bishop Dunstan Maboya kutoka Arusha, Mch. Sylvanus Komba kutoka Dodoma na wachungaji zaidi ya 10 wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Tunakuomba sana usikose maombi haya ni ya muhimu sana kwako na maisha yako kwa ujumla. Mungu atafungua milango ya mafanikio katika kazi yako, biashara yako, masomo yako, mifugo yako, mashamba yako, miradi yako, ajira yako, uzao wa tumbo lako, ndoa yako, familia yako, afya yako n.k

Siku ya Jumapili Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3.



















Comments