08.07.2018: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE PAMOJA NA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHECHENI "B" KWENYE UZINDUZI WA SEMINA YA MID YEAR CROSS OVER WALIOMBEA AMANI TAIFA LA TANZANA

08.07.2018: MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B": KULIOMBEA TAIFA

Katika uzinduzi wa semina ya Mid Year Cross Over 2018 iliyofanyika siku ya Jumapili 08.07.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare, Bishop Dunstan Maboya, Mch. Sylvanus Komba kutoka Dodoma na wachungaji mbalimnali na waumini wa kanisa hilo waliweza kuliombea Taifa la Tanzania amani na utulivu, pia walimuombea Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, viongozi wote wa serikali pamoja na Bunge la Tanzania.

Semina hii ni ya siku 8 ambayo itahitimishwa siku ya Jumapili 15.07.2018 kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Siku za katikati ya wiki semina inaanza saa 9:30 alasiri. Lengo la Semina hii ni kumshukuru Mungu kwa miezi sita iliyopita na kumkabidhi Mungu miezi sita iliyobaki kumaliza mwaka 2018. 

Semina hii hufanyika mara moja tu kwa mwaka kwahiyo si ya kukosa kabisa. Watu wengi sana wanapokea miujiza yao kutoka kwa Mungu baada ya kutamkiwa baraka na watumishi wa Mungu. Wanenaji katika semina hii ni Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare, Bishop Dunstan Maboya, Mch. Sylvanus Komba kutoka Dodoma, mchungaji kutoka Uganda na wachungaji zaidi ya 10 kutoka katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiliombea Taifa la tanzania pamoja na Rais.















Comments