08.07.2018: BIBI ATOA MCHANGO WAKE WA MBUZI SIKU YA UZINDUZI WA SEMINA YA MID YEAR CROSS OVER 2018

Katika uzinduzi wa semina ya siku 8 ya Mid Year Cross Over 2018 uliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 08.07.2018, tulishuhudia bibi akitoa mchango wa mbuzi baada ya kutambua umhimu wa huduma inayotolewa na kituo cha PRAISE POWER RADIO 99.3fm na jinsi anavyolipenda kanisa lake la Mlima wa Moto Mikocheni "B" pamoja na watumishi wake.

Kumbuka kituo cha Praise Power Radio kimekumbwa na tatizo la uchakavu wa "Transmitter" ambayo inasaidia kurusha matangazo kwa masafa marefu. Kwahiyo waumini na wadau wa Praise power Radio 99.3fm wamekuwa wakijinyima kwa kutoa kile walichonacho kuhakikisha chombo hicho kinapatikana kwa haraka ili watu wapate kumjua huyu Mungu kupitia Praise Power Radio 99.3fm. 

Hakika bibi huyu alionyesha ni jinsi gani anampenda Mungu na kulipenda kanisa lake kwa kujinyima kwaajili ya kazi ya Mungu. Naamini mchango wake huu utasaidia watu wengi sana kumjua huyu Mungu na kuokoka pale tu watakapokuwa wakisikiliza Praise Power Radio 99.3fm.

Baada ya kutoa mchango wake, wachungaji waliweza kumuombea na kumtamkia baraka. Tunakuomab na wewe uzidi kumuombea huyu bibi yetu ili Mungu ampe maisha marefu na kuendelea kumtolea Mungu bila kuchoka.

Sasa nikualike wewe katika semina hii ya Mid Year Cross Over 2018 ambayo hufanyika mara moja tu kwa mwaka. Na semina hii kwa siku za katikati ya wiki inaanza saa 9:30 alasiri na siku ya Jumapili ni saa 3 asubuhi hadi 8 mchana. wanenaji ni Bishop Mhe. Dr. Gerttrude Rwakatare, Bishop Dunstan Maboya, Mchungaji kutoka Uganda, Mch. Sylvanus Komba na wengine wengi. Ni siku 8 za Kumshukuru Mungu kumaliza miezi sita na kumkabidhi Mungu miezi sita iliyobaki kumaliza mwaka 2018. Tunawakaribisha watu wote.











Comments