08.07.2018: BAADHI YA WATU WALIOKOKA SIKU YA KWANZA YA SEMINA YA MID YEAR CROSS OVER YA

Baadhi ya watu walioamua kuokoka siku ya kwanza ya Semina ya Mid Year Cross Over 2018  iliyofanyika siku ya Jumapili 08.07.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Mch. Francis Machichi aliwaongoza sala ya toba na baadae wachungaji waliweza kuombewa hawa waongofu wapya. Mungu aliweza kuwafungua kutoka katika nguvu za giza na mapepo yaliyokuwa yakiwasumbua kwa kipindi kirefu.  baada ya kuombewa walibatizwa kwa maji mengi na kujazwa na Roho Mtakatifu. Siku ya Jumatatu na Jumanne ni siku zao za kuanza mafundisho ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 9 alasiri.

Kumbuka semina hii Kumshukuru Mungu kwa miezi sita iliyopita na kukabidhi nusu mwaka kwa Mungu itahitimishwa siku ya Jumapili 15.07.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". siku za katikakti ya wiki itakuwa ikianza saa 9:30 alasiri na siku ya Jumapili itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Wanenaji na Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare, Bishop Dunstan Maboya, Mch. Sylvanus Komba na Apostle Francis Musili kutoka Kenya.


TUONE BAADHI YA SABABU ZA WATU KUOKOA
1. Kuurithi uzima wa milele.

Yohana 3:16-18 '' Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU.''

2. Tumtumikie YESU KRISTO.
Yohana 12:26 '' Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, BABA atamheshimu.''

3. Tuishi maisha Matakatifu.
1 Petro 1:15-16 '' bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.''


4. Tuwe kielelezo cha matendo mema kwa watu wote.
1 Tiomotheo 1:16 ''Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristo audhihirishe uvumilivu wake wote; niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini baadaye, wapate uzima wa milele.''

5. Tuwalete wengine kwa YESU.
Mathayo 10:7-8 ''Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure. ''

6. Tumeokoka ili tuwe na ushirika na ROHO MTAKATIFU.
2 Kor 13:14 '' Neema ya Bwana YESU KRISTO, na pendo la MUNGU, na ushirika wa ROHO MTAKATIFU ukae nanyi nyote.''

7. Tumeokoka ili tuufundishe ulimwengu jinsi ya kumwabudu MUNGU aliye hai.
Zaburi 29:2 ''Mpeni BWANA utukufu wa jina lake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu.''

Usipange kukosa semina hii. Usafiri wa kufika kanisani siku za katikati ya wiki ni bure kuanzia Mwenge kwenye mtaa na siku ya Jumapili usaifi utakuwa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3


Mch. Francis Machichi
















































































































































Comments