01.07.2018: TUMSHUKURU MUNGU HATA KWENYE MAPITO MAGUMU

Kuna wakati unapitia magumu, unawaza sana, unaangalia kulia na kushoto huoni mtu wa kukushika mkono lakini leo natamani ni kwambie kuwa, hata kama unapitia magumu ya aina gani usimuache huyu Yesu Kristo kwani yeye ndiye mfariji wetu, ndiye anayefungua milango ya mafanikio katika mapito tunayopitia. Huyu Yesu hajawahi kumuacha mtu akiteseka bila sababu bali kila aliyemuita kwa kumaanisha aliitika na kumsaidia.

Tusiwaangilie sana wanadamu katika mapito yetu na tukamsahau huyu Yesu Kristo kwasababu wanadamu watakushika mkono kwa muda tu na baadaye watakuachia lakini Yesu akiamua kukushika mkono hakuachi kamwe mpaka mwenyewe uamue kumuacha. Wengi waliong'ang'ania mkono wa Yesu waliona mafanikio makubwa katika maisha yao na mipango yao iliwanyookea. 

Kwako wewe unayepitia magumu kipindi hiki, Mungu akusaidie, akuvushe hapo ulipo, akushike mkono, akuvute katika shimo la mateso, akupe faraja kipindi hiki kigumu unachopitia. Ombi langu kwako ni kujisogeza kwa huyu Yesu Kristo kipindi hiki kigumu unachopitia na nyenyekea kwake. Na ili ushikwe mkono ni wewe kuachana na maovu na kutenda yaliyo mema kama anavyotuelekeza katika kitabu kitakatifu yaani Biblia.

Usithubutu kuwaza mabaya katika hayo mapito yaliyokukuta, huwezi jua Mungu amekuepusha na mangapi. Usiwaze kumkufulu Mungu kutokana na changamoto zako. Acha mawazo potofu yatakayosababisha ukatumbukia katika matatizo makubwa zaidi ya hayo.

Yawezekana toka jana hujala chakula, njaa inakuuma na huoni wa kukupatia chakula au ywezekana umeambiwa kesho uhame katika nyumba hiyo ya kupanga kwa kukosa kodi, yawezekana umepewa barua ya kufukuzwa kazi na boss wako, yawezekana umeletewa habari mbaya za kusikitisha na mambo mengine mabaya kama hayo, lakini mimi nataka nikuambie kuwa, Mungu anajua mapito yako na yupo tayari kukusaidia na hayo yote. Usijaribu kuwaza mabaya kutokana na hayo mapito yako bali inua macho yako kwa Mungu na peleke mashitaka yako. Mungu ana njia nyingi sana za kusaidia watu wanaoita magumu kwahiyo "anytime" Mungu anaweza kukurudishia furaha yako.

Pengine umeondokewa na yule uliyempenda na imefika kipindi huoni mtu atakayeweza kuziba pengo hilo, mimi nataka nikuambie kuwa Mungu anajua cha kufanya juu yako kutokana na hilo pengo lako, anajua ni jinsi gani anaweza kukupa faraja na ukaishi maisha yako ya amani kama awali, kwahiyo usithubutu kutamka kibaya juu ya kuondokewa na ndugu au jamaa yako. Jiulize ni watu wangapi waliofariki na uliumia sana, lakini baada ya muda ukayasahau yote na ukaendelea na maisha yako, kwa hiyo hata hilo unalopitia ipo siku litaondoka katika kichwa chako na utaendelea na maisha yako ya kawaida.

Unachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuwa karibu sana na Mungu, kushiriki ibada, kusikiliza Neno la Mungu kupitia media mbalimba, kuwatii watumishi wa Mungu, kuonyesha upendo kwa kila mtu, kuliishi Neno la Mungu, kutumia muda wako kwa kumsifu Mungu kwa njia ya nyimbo, kujitoa kwa kazi ya Mungu, kulitangaza Neno la Mungu mtaani kwako au mhali popote pale, kufanya toba, kufunga na kuomba, kuujenga mwili wa Kristo kwa utoaji kanisani kwako na kutenda yale yote yaliyomema mbele za Mungu na mbele za wanadamu.

Mwisho, nikualike kanisani wewe ambaye ulikosa ibada ya Jumapili 01.07.2018 ya MAOMBI YA HATARI YA KUBOMOA NGOME ZILIZOZUIA KUFKIA MALENGO YAKO NA KUKOMESHA LAANA ZOTE iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. 

Katika ibada hii tutakuwa na kipindi cha maombi, kipindi cha Sunday School, Kipindi cha kuwaombea na kuwaongoza sala ya toba watu wanaokoka, kipindi cha kusifu na kuabudu, Kipindi cha Neno la Mungu na Maombezi n.k

Siku ya Jumapili usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3 


















Comments