01.07.2018: NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE. DKT. MARY MWANJELWA AKIOMBEWA KATIKA IBADA YA MOMBI HATARI YA KUBOMOA NGOME ZINAZOZUIA KUFIKIA MALENGO YETU NA KUKOMESHA LAANA ZOTE


Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa siku ya Jumapili 01.07.2018 kwenye ibada ya MOMBI HATARI YA KUBOMOA NGOME ZINAZOZUIA KUFIKIA MALENGO YETU NA KUKOMESHA LAANA ZOTE iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare, wachungaji na waumini wote waliweza kumuombea mheshimiwa Dr. Mary Mwanjewa ambaye amekuwa kiongozi bora sana katika kazi yake ya kusimamia masuala ya kilimo Tanzania.

Mheshimiwa Dr. Mary Mwanjewa ameungana na wana Mlima wa Moto Mikocheni "B" katika maombi ya siku 7 ya kufunga na kuomba yaliyoanza Jumapili, na pia aliomba Watanzania wote kumuombea Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi yake ya kuliongoza Taifa la Tanzania. Na mwisho alihitimisha kuwashukuru waumini wa kanisa hilo kwa maombi yao na kusisitiza kuliombea Taifa la Tanzania na viongozi wake.

Yawezekana wewe ni kiongozi katika familia yako, kata yako, kitongoji chako, wilaya yako, mkoa wako n.k na ungehitaji maombi kwaajili ya ulinzi katika kazi yako; Tunakualika katika ibada ya Jumapili hii kanisani Mlima wa Moto Mikocheni "B" ili tukufanye maombi ya hatari dhidi ya maadui zako wanaokesha kukuombea mabaya kwa waganga na wachawi. Sio kila mtu anatamani kukuona katika nafasi uliyo nayo, au kipato unachopata kazini kwako, au kazi unayofanya, au kibali ulichonacho kwa mkubwa wako kazini, au heshima uliyonayo mabosi wako au wafanyakazi wenzako, au mafanikio uliyonayo kutokana na kazi nzuri unayofanya hapo kazini kwako  au promosheni unazozipata kazini kwako n.k. Kila mtu anapigana na wewe kuhakikisha unarudi nyuma, kwahiyo ili kuepukana na vipingamizi mbalimbali katika kazi yako, kimbilia kwa Yesu Kristo na kutana na watumishiwa Mungu hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" ambao Mungu anwatumia sana kuokoa maisha ya watu yasiangamie na yule muovu. Ibada siku ya Jumapili itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usikose.

















Comments