01.07.2018: MARTHA KOMANYA ALIVYOONGOZA KIPINDI CHA KUSIFU NA KUABUDU KATIKA IBADA YA MAOMBI HATARI YA KUBOMOA NGOME

ZABURI 20:7. "Hawa wanataja magari na hawa wanataja farasi, Bali sisi tunalitaja jina la BWANA, Mungu wetu."

Hivi ndivyo wana Mlima wa Moto Mikocheni "B" walivyolitaja jina la BWANA, Mungu wetu kwa kumuimbia nyimbo zenye kulisifu jina la BWANA wetu aliye hai siku ya Jumapili ya kwanza ya mwezi wa saba ya tarehe 01.07.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwenye ibada ya KUONDOA NGOME ZINAZOZUIA KUFIKIA MALENGO NA KUANGAMIZA LAANA ZOTE. Ilikuwa ni ibada iliyotawaliwa na uwepo wa Mungu na watu walifunguliwa na kupokea baraka za Mungu..

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mtumishi wa Mungu Martha Komanya pamoja na Praise and Worship Team kwa kutuongoza katika kipindi cha kusifu na kuabudu. Mungu alishughulika na watu wenye uhitaji kupitia ibada hii.

Wewe ambaye ulikosa ibada ya Jumapili tunakualika katika ibada ya Jumapili hii itakayofanyika hapa kanisani- Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Walete wenye shida mbalimbali, na BWANA atashughulika nao kupitia watumishi wa Mungu ambao watawaombea na kuwatamkia baraka. Wengi walioamini na kuchukua hatua ya kufika kanisani, Mungu ahakuwanyima kile walichokiomba. Na wewe ukiamini na kuchukua hatua ya kufika mahali hapa BWANA ataangilia haja ya moyo wako na kukushika mkono wenye kukuondoa hapo ulipo na kufikia hatma ya malengo yako.

Martha Komanya
































Comments