01.07.2018: MAOMBEZI YA HATARI YA KUBOMOA NGOME ZILIZOZUIA USIFIKIE MALENGO YAKO YALIVYOFANYIKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Siku ya Jumapili 01.07.2018 kulifanyika ibada ya maombi hatari ya kubomoa ngome zilizozuia kufikia malengo yetu. Maombi haya yalifanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" yakiongozwa na mtumishi wa Mungu Bishop Mhe. Dr. Gertrude Rwakatare akishirikiana na wachungaji zaidi ya 10 wa kanisa hilo. Kila mtu aliweza kupata nafasi ya kupeleka maombi yake kwa Mungu kulingana na lile linamsumbua katika maisha yake. Maombi haya yalikuwa ya hatari sana, tulishuhudia watu wakitokwa na mapepo na nguvu za giza huku wakipiga kelele. BWANA aliingilia kati kuhakikisha watu wanaachiliwa kutoka katika mikono ya adui shetani na kuwa katika mikono salama ya Mungu. 

Kuna baadhi ya watu waliwekewa ngone na maadui zao ili wasipate kazi, watoto, mimba, kibali, mafanikio, promosheni, afya bora, elimu nzuri, ada ya shule, kodi ya nyumba, viwanja, kujenga nyumba zao, wasimalizie ujenzi na mengine kama hayo, lakini tunamshukuru Mungu kwa maombi ya Jumapili watu wengi walifunguliwa na sasa wanafurahia ukuu wa Mungu. Unajua unapojiachilia kwa Mungu, na ukimwamini na kutimiza yale anayokuagiza katika kitabu chake kitakatifu, Naye hatakuacha katika mateso, bali atahakikisha anakuondoa katika shimo na maadui zako na kukuficha katika mbawa zake. 

Hakika Mungu ni mwema sana kwa wale wamuaminio na wenye bidii ya kumtafuta. Amua sasa kubadilisha "style" ya maisha uanayoishi, muangalie huyu Mungu wa mbinguni kwa kumtumikia, kufanya yale anayokuagiza, kuwasikiliza na kuwatii watumishi wake, kuwasaidia wenye uhitaji, kuwa na upendo kwa kila mtu, kushiriki ibada kila kuitwapo leo, kumtumikia Mungu kwa karama au kipaji ulichonancho, kutoa zaka, kushika amri kumi za Mungu na kuzifanyia kazi, kusoma sana Neno la Mungu na kuliishi katika maisha yako ya kila siku, kutubu dhambi zako kila wakati, kutenda yaliyo mema na yenye kumpendeza Mungu, kufunga na kuomba na mengine kama hayo. Utakapofanya haya yote Naye BWANA atanyoosha mkono wake wa rehema na kukuvuta kwake na maisha yako yatakuwa salama na yenye mafanikio

Wewe unayepitia changamoto mbalimbali katika maisha yako, tunakualika katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Walete wenye shida mbalimbali, na BWANA atawaponya na kuwafungua katika vifungo vyao. Mungu ni mwaminifu sana kama utamkubali na kumtumikia kwa uaminifu.

Siku ya Jumapili usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3
Bishop Hon. Dr. Gertrude Rwakatare




Mch. Mainah kutoka Kenya



Mch. Francis Machichi















































Mzee wa Kanisa mama Mramba



















































Mch. Stanley Nnko






















Comments