01.07.2018: BAADHI YA WATU WALIOAMUA KUOKOKA KATIKA IBADA YA MAOMBI HATARI YA KUBOMOA NGOME ZILIZOZUIA KUFIKA MALENGO YETU

Baadhi ya watu walioamua kuokoka na kumpokea Yesu Kristo kuwa BWANA na Mwokozi wa maisha yao siku ya Jumapili 01.07.2018 kwenye ibada ya MOMBI HATARI YA KUBOMOA NGOME ZINAZOZUIA KUFIKIA MALENGO YETU NA KUKOMESHA LAANA ZOTE iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Mch. Manumbu aliwaongoza sala ya toba na baadae waliweza kuombewa na kutamkiwa baraka katika maisha mapya ya wokovu watakayoanza kuyaishi baada ya kubatizwa kwa maji mengi. Baada ya maombezi kumalizika walibatizwa kwa maji mengi na kujazwa Roho Mtakatifu kama vile Yesu Kristo alivyobatizwa kwa maji mengi na Yohana Mbatizaji. Siku ya Jumatatu na Jumanne ni siku zao za kuingia darasani kwaajili ya masomo ya kukulia waokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". masomo yanaanza saa 9:30 alasiri.

Yawezekana unatamani kumrudia mUngu wako, unahitaji kutubu dhambi zako, unahitaji kuombewa, unahitaji kubatizwa na unahitaji kujifunza Neno la Mungu litakalokusaidia kumjua sana Mungu, tunakualika katika ibada ya Jumapili hii, ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.




Mch.Manumbu








































Comments