24.06.2018: WATU WAZIDI KUTOA MICHANGO YAO KWAAJILI YA KUNUNUA TRANSMITTER YA KITUO CHA REDIO CHA PRAISE POWER 99.3FM

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa jinsi watu wanavyozidi kujinyima kwaajili ya kusaidia kazi ya Mungu kusonga mbele. Tangia tangazo limetolewa la kuchangia ununuzi wa "Transmitter" ya kituo cha redio ya PRAISE POWER 99.3FM ambayo inajihusisha na kutangaz abari za Mungu (habari Njema), watu wamekuwa mstari wa mbele kufanya wawezalo kuhakikisha kifaa hicho kinapatikana kwa haraka. Kwa muda wa miaka ya 15 tangia kituo hiki kianze huduma ya kutangaza habari za Mungu hakiwajawahi kubadilisha kifaa hicho (Transmitter) kinachosaidia kurusha matangazo kwa masafa marefu, na mwaka huu 2018 kifaa hicho kimefikia mahali kinahitajika kubadilishwa kutokana na uchakafu na kusababisha matangazo kutowafikia wahusika kwa usikivu mzuri.

Tunapenda kukushukuru wewe ambaye umeguswa na jambo hili na umekuwa ukijinyima kupata mahitaji yako na kuamua kujitoa kwaajili ya kazi ya Mungu. Hii inaonyesha ni kiasi gani umetambua mchango wa kituo hiki cha redio kwa familia yako na jamii yako kwa ujumla.

Kupitia kituo hiki cha Praise Power Redio 99.3fm watu wengi wamefunguliwa, wameokoka, wamemrudia Mungu, wameponywa, wamepata miujiza yao, wametangaza huduma zao, wamefarijiwa, wamejifunza Neno la Mungu, wameingiwa na hofu ya Mungu, wameacha dhambi, wameacha uhalifu na mengine kama hayo baada ya kupata mafundisho, maombezi, masomo na mahubiri kutoka kwa watumishiwa wa Mungu mbalimbali.

Kumbuka kituo hiki cha redio ni kwaajili ya dini zote za Kikristo, waimbaji kutoka madhehebu mbalimbali, watumishi wa Mungu kutoka katika makanisa yao, walimu wa maswala ya kidini n.k. Ni kituo kisichobagua dini ya mtu ya Kikristo, kabila la mtu, Taifa la mtu na rangi ya mtu bali ni kituo cha watu wote wenye nia ya kutangaza habari njema za Kristo.

Tuna kila sababu ya kuwashukuru viongozi wa kituo hiki, watangazaji, wafanyakazi, wateja wetu, wasikilizaji na kila mtu anayehusika kwa njia moja au nyingine kwa mchango wao mkubwa wa kujitoa kwaajili ya kuhakikisha redio hii inakuwa bora kwaajili ya kuokoa maisha ya watu na kuwaleta watu kwa Mungu.

Wewe ambaye unaguswa na changamoto inayopitia redio hii, unaweza kuwakilisha mchango wako siku ya Jumapili katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Ni maombi yangu Mungu akakuwezeshe kupata nafasi ya kufika hapa kanisani, akusaidie kupata nauli, akusaidie kupata mafuta ya kujaza kwenye gari lako, akuwezeshe kupata afya njema, akuwezeshe kutopata kipingamizi siku ya Jumapili ili usifike kanisani, akuwezeshe kupata mchango wako kwaajili ya ununuzi wa "Transmitter" ili watu wengi waokoke kupitia kituo hiki cha redio. Mchango wako utasaidia sana kuokoa maisha ya watu na Mungu hatakuacha kwa hicho utakachokifanya siku ya Jumapili.

Mungu akubariki sana.
Siku ya Jumapili usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3

Mch. Stanley Nnko wakiwapongeza watu wanaojitoa kutoa michango yao


































Comments