24.06.2018: MCH. PRISCA CHARLES NA WAUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" WALIPOMSIFU MUNGU SIKU YA JUMAPILI

Mithali 150:1-2: "Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake. Msifuni kwa matendo yake makuu. Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake."

Hivi ndivyo waumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" walivyoweza kumsifu Mungu katika ibada ya "Kurudishiwa Utakatifu Ulioibiwa na Kuvishwa vazi la Utukufu" iliyofanyika siku ya Jumapili 24.06.2018 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Mch. Prisca Charles akishirikiana na Praise & Worship Team ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" waliweza kuongoza kipindi cha sifa.

Watu waliweza kupata nafasi nzuri ya kumsifu Mungu kutokana na matendo makuu ambayo amekuwa akifanya katika maisha ya watu kwa wiki nzima. Kabla ya kipindi cha kusifu watumishi wa Mungu waliweza kulitakasa kanisa kwa maombi ili eneo la sifa liwe takatifu, kama tunavyosoma katika Mithali 150:1 " Msifuni Mungu katika patakatifu pake...."

Mungu wetu ni Mkuu anastahili sifa na utukufu. Mungu wetu anatutendea mema kila kuitwapo leo. Mungu wetu ni Mungu wa watu wote bila kujali kabila la mtu, umaarufu wa mtu, utajiri wa mtu, hali ya mtu, rangi ya mtu, umri wa mtu n.k. yeye ni Mungu wa kila mtu kwahiyo tunapaswa kumuabudu na kumsfu kwa yale anayotutendea.

Kama watoto wake tunahitajika kumsifu kwa roho wa kweli na tusiwe ni watu wa kufuata mikumbo katika ibada ya sifa. Kile tunachokiimba tunapaswa kukimaanisha na tusiwe watu wa kuimba bila kumaanisha. Yale tunayoyaimba tunapaswa kuyafanyia kazi katika maisha yetu.

Mungu wetu anatamani sana kuona watoto wake wanatenga muda wao na kuacha kila kitu kwaajili yake. Katika mambo makubwa ambayo Mungu anapenda ni kuona watu wanamsifu.

Wewe amnaye ulikosa ibada hii, tunakualika katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3

Mch. Prisca Charles














Comments