25.05.2018: WATU WALIVYOMSIFU MUNGU KATIKA IBADA YA KUIOMBEA FAMILIA - MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

// ZABURI 90:1-4: Wewe BWANA, umekuwa makao yetu, kizazi baada ya kizazi. Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, na tangu milele hata milele ndiwe Mungu. Wamrudisha mtu mavumbini, usemapo, Rudini, enyi wanadamu. Maana miaka elfu machoni pako ni kama siku ya jana ikiisha kupita na kama kesha la usiku. //

Mungu wetu wa mbinguni anapenda sana kuona watoto wake aliowaumba na kuwaweka duniani wakimsifu kwa maneno mazuri au kwa nyimbo nzuri zenye kumtukuza kwa kazi yake njema.

Kuna maneno mengi sana unaweza kuyatumia kumsifu Mungu na sio lazima uyashike kwa kukariri kutoka kwenye vitabu. Mungu amekupa kinywa na sauti nzuri ya kumsifu Yeye. Kwahiyo katika maisha yako jitahidi kutenda muda kwaajili ya kumsifu Mungu tu kwa kunena au kuimba. Mpe sifa zake Mungu kwa kile anachokifanya katika maisha yako, familia yako, kiji chako, wilaya yako, mkoa wako, jiji lako, Taifa lako na bara lako. Unaweza kumsifu kwa uumbaji wake na kazi zake anazofanya katika viumbe vyake, mimema yake n.k.

Kwa kutambua hilo waumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" waliweza kutenga muda wao kwaajili ya kumsifu Mungu kwa njia ya uimbaji wakiongozwa na Mch. Prisca Charles na Praise & Worship Team ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 20.05.2018 katika ibada ya KUIOMBEA FAMILIA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Waumini walionekana kuguswa na tendo hili la kumsifu Mungu, kwani sura zao zilichangamka zikiwa na furaha kutokana na uwepo wa Mungu uliosambaa katika kanisa hilo na nguvu za Mungu zilivyokuwa zikiwaguza na kuwapoa nguvu za kuendelea kumsifu Mungu aliye hai. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare naye hakuwa nyuma katika zoezi la kumsifu Mungu kwa kuimba na kucheza. Yaani ilikuwa ni ibada ya kuchota baraka kutoka kwa Mungu kupitia ibada ya kusifu na kuabudu.

Unapokuwa kanisani kwaajili ya ibada ya kusifu, unachotakiwa kukifanya ni kumsifu Mungu kwa Roho wa kweli na usiwe mtu wa kuigiza, unapoimba unatakiwa kumaanisha kutoka ndani ya moyo wako na usiwe ni mtu wa kukariri maneno, unatakiwa kutozea ibada ya kusifu bali ifanye ni siku yako ya kwanza ya kumsifu Mungu, usipende kulazimishwa kuimba au kupiga makofi kutoka kwa kiongozi wako anayeongoza kipindi cha sifa bali muombe Mungu usukumwe mwenyewe kumpigia makofi na kupigia vigeregere Mungu wako kwa kupenda kulingana na jinsi ulivyoguswa na wimbo, unapoimba mtazame Mungu na sio kuangalia watu wengine wanaimbaje, usikatishwe tamaa na mtu yeyote eti huwezi kuimba au huna sauti nzuri ya kuimba au hujui kucheza, unapoimba na kucheza jitahidi kuwa ana adabu kwasababu unayemuimbia ni mkuu kuliko kitu chochote duniani na mbinguni.

Yawezekana ulikosa ibada ya Kuiombea Familia, na ungetamani mtumishi wa Mungu aseme jambo juu ya familia yako, basi usikose ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.


Usafiri wa kufika kanisani ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola, Ilala Stand, Tegeta Wazo, Goba Stand, Mbezi Mwisho/Kimara Stop Over, Buguruni Chama/ Mandela Road, Mbagala Rangi 3


Mch. Prisca Charles




Mch. Prisca Charles










































































Comments