25.05.2018: MAOMBI YA KUIOMBEA FAMILIA YAFANYIKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

TAFAKARI NENO HILI NA LIFANYIE KAZI.
"MITHALI 4: 20-25: Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu. Zisiondoke machoni pako; Uzihifadhi ndani ya moyo wako. Maana ni uhai kwa wale wazipatao, na afya ya mwili wao wote. . Linda moyo wako kuliko yote ulindao; Maana ndiko zitokako chemichemi za uzima. Kinywa cha ukaihidi ukitenge nawe, na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe. Macho yako yatazame mbele, na kope zako zitazame mbele yako sawasawa.//

Mungu wetu anatamani sana kuona familia zetu zinalinda mioyo yao kwa mambo mema maana huko ndiko zitokako chemichemi za uzima. Moyo wako ukiacha kufanya kazi basi na uhai wako unaishi hapo hapo. Familia zetu zikiwa na matendo mabaya basi familia hizi kumuona Mungu ni vigumu ila kuingia jehanamu kwao ni rahisi sana kwasababu matendo mabaya ni ya shetani na sio ya Mungu.. Kwahiyo familia zetu zikihitaji kuishi maisha marefu basi zinapaswa kulinda mioyo yao kuliko vyo ilindayo maana huko ndiko chanzo cha uzima. Familia zetu zinatakiwa kuyatenda yaliyo mazuri mbele za Mungu na mbele za wanadamu ili siku ya mwisho ya kuishi hapa duniani zikamuone Mungu aliye hai huko mbinguni.

Familia zetu zinatakiwa kujitenga na vinywa vya ukahidi na midomo ya upotovu ambayo kazi yake ni kunena yaliyo maovu na yenye kuleta chuki na uhasama katika familia. 

Tunamshukuru sana Mungu kwa siku ya Jumapili 20.05.2018 katika ibada ya maombi ya KUIOMBEA FAMILIA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", tuliona Mungu akishughulika na maisha ya watu kupitia maombi, kwani kila mtu alimuomba Mungu kulingana na matatizo anayokumbana nayo katika familia yake. Kuna watu wengine katika familia wamekumbwa na magonjwa ya kurithi, kutopata wachumba, kutooa wala kuolewa, kukataliwa, umaskini, umalaya, uzinsi, uasherati, ulevi, kunywa madawa ya kulevya, madeni, kukosa kazi, mikosi, ajali, nguvu za giza, kuota ndoto mbaya, watoto kutowaheshimu wazazi wao, kukosa amani katika ndoa, kutopandishwa vyeo wala mishahara, kutelekeza watoto, uongo, majivuno, wizi na mengine kama hayo. Kwahiyo kila mtu aliingia katika maombi kufunga kila balaa na mikosi katika familia yake.

Katika maombi haya watu walifunguliwa kutoka katika nguvu za giza zilizokuwa zikiwasumbua kwa muda mrefu. Tulishuhudia watu wakitokwa na mapepo baada ya kukutana na nguvu za Mungu kupitia watumishi wake. Watumishi mbalimbali waliweza kuwagusa watu na kuziombea familia zao ili zifunguliwe kutoka katika mateso na shida zao za muda mrefu. Mungu wetu ni wa huruma maana amekuwa akisikiliza maombi ya wana Mlima wa Moto Mikocheni "B" na kujibu kwa moto. Kila anayeingia na mizigo katika kanisa hili amekuwa akitoka akiwa mwepesi maana mizigo yote imeondolewa katika maisha yake.

Tunachokiomba kwa wewe ambaye umefunguliwa katika shida zako, macho yako na kope zako zimuangalie Mungu tu, acha kurudi nyuma bali songa mbele kwa kuyatenda yaliyo mema mbele za Mungu na mbele za wanadamu. Utakaporudi nyuma tu utakumbana na mabaya makubwa zaidi ya yale ya mwanzo.. Familia yako itakumbwa na mikosi na balaa kama utayarudia matapishi uliyotapika awali. Anza sasa kumtazama huyu Yesu Kristo kwa kutenda yaliyo mema, shiriki ibada, soma Neno la Mungu na uliishi, saidia watu, funga na kuomba, fanya toba, onyesha upendo kwa kila mtu, uwe mtoaji kanisani, toa fungu lako la kumi na zako yako kwa uaminifu n.k. Kama utayafanya haya kwa uaminifu utaona Mungu anavyokushangaza katika kila hatua ya maendeleo yako pamoja na kuilinda familia yako.

Yawezekana ulikosa ibada hii na unatamani sana Familia yako ifanyiwe maombi maalum, tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare













 Mch. Mwakibete

 Mch. Stanle Nnko
 Mch. Mainah
Mch. Francis Machichi



Mch. Manumbu





Mch. Asenga























































Comments